MAGAIDI NCHINI MALI KUKIONA, QATAR YAONGEZA NGUVU KUPAMBANA NAO

Bamako, MALI.

Serikali ya Qatar imesema kuwa imetuma nchini Mali magari ishirini na nne (24) ya kijeshi kwa lengo la kile ilichokitaja kuwa kuzisaidia nchi za Afrika za eneo la Sahel kuendesha vita dhidi ya ugaidi.

Hayo yameelezwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo na kuongeza kuwa, magari hayo ya kijeshi yatasaidia vita dhidi ya ugaidi na kudhamini hali ya usalama si nchini Mali pekee bali katika nchi zote za eneo la Sahel zinazojulikana kwa jina la G5.

Nchi hizo za G5 ambazo ni Mali, Burkinafaso, Niger, Chad na Mauritania mwaka jana ziliasisi kikosi cha askari wa kuendesha operesheni dhidi ya ugaidi. Wakati huo huo Saudi Arabia na Imarati zimekubali kukipatia kikosi hicho cha Sahel dola zisizopungua milini 150.

Qatar imezidisha jitihada za kujidhihirisha kuwa ni nchi inayoweza kuwa na nafasi muhimu katika suala la usalama wa kimataifa tangu nchi nne za Kiarabu yaani Misri, Imarati, Bahrain na Saudi Arabia ziiwekee vikwazo vya kila upande vikiwemo vya kidiplomasia na kususia uchumi wake mwezi Juni mwaka jana.

Nchi hizo ziliituhumu Qatar kuwa inaunga mkono ugaidi. Ndege za kijeshi za Qatar ndizo zilizosafirisha magari hayo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.