MAGAIDI 27 WAUAWA NA VIKOSI VYA ULINZI VYA MISRI HUKO SINAI

Cairo, MISRI.

Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Misri vimewauwa magaidi wapatao ishirini na saba (27) katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika eneo la Sinai la Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kamanda mkuu ya vikosi vya ulinzi vya Misri jana alitangaza kuwa wanajeshi pamoja na wahandisi wa kijeshi walinasa na kuripua mabomu 344 ambayo magaidi walikuwa wameyatega ili kuwalenga askari jeshi na wale wa usalama wa nchi hiyo, na walifanikiwa kuangamiza maficho 342 ya magaidi huko kaskazini na katikati mwa eneo la Sinai.

Idadi kubwa ya miripuko na silaha mbalimbali zilinaswa pia katika operesheni hiyo ya jana Jumatano na jeshi la Misri katika maficho ya magaidi hao wa Daesh (ISIS) huko Sinai.

Mapigano kati ya askari usalama wa Misri na watu wenye silaha katika mkoa wa Sinai Kaskazini yalishika kasi mwaka 2014 tangu aingie madarakani huko Misri Rais Abdel Fattah al Sisi.

Kundi la kigaidi linalojiita Daesh lililopo wilaya ya Sinai nchini humo limekuwa likiendesha hujuma katika mkoa huo na limeshauwa makumi ya watu katika operesheni zake dhidi ya raia na vikosi vya ulinzi vya Misri.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.