MACHAR AGEUKWA NA WAASI WAKE, WAKATAA MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA KUMREJESHA KATIKA WADHIFA WAKE

JUBA. Nchini Sudan Kusini kikundi cha Waasi kinachomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Riek Machar leo kimeukataa mpango wa amani ulioafikiwa wa kumrejesha kiongozi wao huyo kwenye umakamu wa rais, wakisema makubaliano hayo hayajapunguza mamlaka makubwa aliyonayo rais wa nchi hiyo, Salva Kiir.

Machar alikuwa makamu wa Kiir hadi mwaka 2013, wakati tofauti za kisiasa zilipochochea vita ambavyo vimesababisha maafa makubwa nchini humo kwa miaka mitano.

Makubaliano ya kumrudishia Machar wadhifa wa makamu wa rais yaliafikiwa mjini Entebbe, Uganda, mwisho wa wiki iliyopita chini ya upatanishi wa Rais Yoweri Museveni.

Awali msemaji wa Riek Machar alisema kuwa Machar alikubali mkataba huo, lakini naibu msemaji wa kundi la waasi, SPLM-IO, Puok Both Baluang, amesema waasi wanastahili kuteua makamu wawili wa rais chini ya makubaliano hayo ya Entebbe na madaraka ya Kiir yapunguzwe.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.