MABULA AMFAGILIA MHE. MAGUFULI KWA KASI YA UTENDAJI WA TARURA KWENYE MIRADI 10 INAYOGHARIMU BI. 5.8

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula amempongeza Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kwa uanzishwaji wa Wakala wa barabara Mjini na Vijijini TARURA ambacho kimekuwa chapa halisi ya ukombozi kwenye sekta ya miundombinu ya barabara Wilayani Nyamagana kwa kutekeleza miradi 10 yenye thamani ya shilingi 5,822,854,934.00 kwa kasi na kiwango katika mwaka wa fedha 2018 hadi 2019.

Mhe. Mabula akiwa ameambatana na Mjumbe kamati ya siasa CCM wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya Mhe. Witness Makale walilakiwa na mwenyeji wao Meneja TARURA wilaya ya Nyamagana Mhandisi Mohamed na kusomewa taarifa kisha kupata fursa ya kukagua miradi 10 ya ujenzi wa miundombinu ya barabara, Madaraja sanjari na uwekaji wa kalvati. Ambapo Mhe. Mabula alikagua mradi wa uzibuaji Mitaro na Kalavati unaogharimu shilingi 41,827,173.20, barabara ya Mawe Nyamazobe Kesese Nyahingi yenye urefu wa Km 2.27, barabara ya Nyegezi Stand kuelekea Malimbe inayogharimu shilingi 293,380,800.00, ujenzi wa barabara ya Buhongwa kuelekea Bulale inayogharimu shilingi 131,844,700.00

Kisha Mhe. Mabula alizifikia pia barabara za Igoma kuelekea Kata ya Kishiri inayogharimu 393,273,450.00, ujenzi wa Makalvati na Madaraja, barabara ya NilePerch kuelekea Mahina Kati hadi Mkuyuni, barabara ya Ipuli kuelekea Igelegele Shule ya Msingi inayojengwa kwa kiwango cha Lami na kugharimu shilingi 587,618,500.00 kisha akamalizia ukaguzi wa daraja la Fumagila linalogharimu shilingi 357,035,550.00 pamoja na mradi wa uwekaji Taa za barabarani katika barabara za Halmashauri ya Jiji la Mwanza inayoghalimu shilingi 317,170,000.00.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.