MAANDAMANO YA BARAZA LA VIJANA(BAVICHA)SERENGETI YAZUIWA NA JESHI LA POLISI

Polisi wilayani Serengeti mkoani Mara imezuia maandamano yaliyopangwa kufanyika leo na Baraza la vijana Chadema(BAVICHA)

Barua ya kuzuia maandamano hayo imetolewa na Mkuu wa Polisi wilaya ya Serengeti Mathew Mgema na kusema swala la kusitisha kikokotoo lilifanywa na Rais John Magufuli wakati wa hotuba yake iliyofanyika Disemba 28,2018

Polisi wamesema badala ya kufanya maandamano hayo wameshauriwa kuwasiliana na wananchi wake wa Bunda mjini ili kupanga namna ya kumpongeza Bulaya katika eneo lake hilo la uwakilishi

Hata hivyo mkuu huyo wa Polisi alisema hatua kali zitachukuliwa Kwa wale wote watakaokiuka na kuonyesha dalili za uvunjifu wa Amani

Maandamano hayo yaliyopangwa kufanyika leo Januari 9/2019 yalikuwa na nia ya kumpongeza Mbunge wa Bunda mjini kupitia tiketi ya Chadema Ester Bulaya kwa jitihada zake za kuwatetea wastaafu katika swala la kikokotoo cha asilimia 25

Akizungumzia zuio hilo la Polisi Katibu wa (BAVICHA)Serengeti Fransis Garatwa amekiri kupokea barua hiyo ya katazo la maandamano kutoka kwa Kamanda wa Polisi Wilaya

Garatwa amesema wametii Agizo kama ilivyoagizwa hivyo hawataandamana isipokuwa watafanya hivyo endapo vijana wa Chama cha Mapinduzi watapewa kibali cha kufanya maandamano kwa jambo kama hilo walilozuiwa

Maandamano hayo yalipangwa kufanyika Leo kuanzia ofisi za chama hicho hadi ofisi za Mbunge wa viti maalum Catherine Ruge(Chadema) na yangepokelewa na mwenyekiti wa chama wilaya

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.