LULA AAPA KUPAMBANA DHIDI YA UAMUZI WA MAHAKAMA KUTOWANIA URAIS

 

Brasilia, BRAZIL.

Rais wa zamani wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva, ambaye anatumikia kifungo cha miaka 12 kwa madai ya rushwa tangu mwezi Aprili mwaka huu, ataendelea na vita yake ya kisheria ili arejeshewe haki ya kuwania katika uchaguzi wa urais mwezi ujao, wanasheria wake wamesema.

Tangazo hili linakuja wakati chama chake cha PT, kimepewa siku chache ambazo mwisho ni leo Jumanne usiku kuteua mgombea mwengine kuchukua nafasi ya Lula kuelekea uchaguzi wa Oktoba 07.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, Mahakama Kuu ya Uchaguzi ilitangaza kwamba Lula hana vigezo kisheria vya kuwania katika uchaguzi wa urais.

Siku ya Jumatatu hapo jana, wanasheria wa Lula na Fernando Haddad, mgombea mwenza, walimtembelea Lula katika jela anakozuiliwa.

Vyanzo vya chama cha PT vimebaini kwamba katika mazungumzo yao Lula alitakiwa kumruhusu Haddad kuwania kwenye nafasi yake na kumpa barua ambapo anawatolea wito wawafuasi wake kumpigia kura.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.