LUGOLA AKABIDHIWA KIJITI NA MWIGULU

Waziri Mpya wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Mhe.Kangi Lugola amekabidhiwa ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba

katika Makao Makuu ya nchi Jijiji Dodoma leo Jumanne, Julai 10, 2018.

Katika ukurasa wake wa Twiter, Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ameandika; “Makabidhiano ya ofisi/kijiti hii leo Dodoma. Nimemtakia kila raheli Mh.Kangi Lugola katika utumishi wake kwa watanzania katika wizara hii.”

Aidha Nchemba mara baada ya kuenguliwa nafasi hiyo alifika jimboni kwake na kuongea na wananchi wake akisema kuwa sasa atapa nafasi ya kuwatumikia vyema wananchi wake.

Mabadiliko hayo ya Baraza  la Mawaziri yalifanywa na Rais John Pombe Magufuli Julia 1, 2018 ambapo alimteua Mbunge wa Mwibara na aliyekuwa Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira, Kangi Lugola kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi akichukua nafasi ya Mwigulu mchemba

Related posts

One Thought to “LUGOLA AKABIDHIWA KIJITI NA MWIGULU”

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.