‘KUFURU NDOA YA DIAMOND NA TANASHA’

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mwanadada Tanasha kutoka pande za Kenya wapo katika mahaba mazito kiasi kwamba wamekuwa wakifuatana kama kumbi kumbi kila mahali.Hali hiyo inaelezwa kwamba ni kutokana na kunogewa na utamu wa penzi lao ambalo bado ni change lakini likiwa na malemgo makubwa katika maisha yao ya baadae
Diamond ambaye ni baba wa watoto watatu Tiffa na Nilan ambao kawapata akiwa na Zari na Mwingine Dylan ambaye kazaa na mwanamitindo ambaye pia ni mwanamuziki Hamisa Mobetto inaonekana kukolea vilivyo kwa binti huyo mkenya ambaye pia ana uraia wa Italia.
Lakini yote kwa yote funga kazi ni kwamba baada ya mahangaiko ya muda mrefu na kupitia mahusiano na wanawake tofauti Diamond anaonekana ni Dhahiri atafunga ndoa na binti huyo wa kikenya Hivyo kufuata nyayo za wasanii wenzake kadhaa wakiwemo AY na hasimu wake katika muziki Alikiba ambao wameoa nje ya Tanzania
Ikumbukwe kwamba safari ya mapenzi ya Diamond ilianzia kwa aliyewahi kuwa miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu ambapo mara mbili walivishana pete za uchumba pasipo kuoana,huku pia mwanamama kutoka Uganda Zarina Hassan na Hamisa Mobetto wakipitia wakipata nafasi ya kutembea na bosi huyo wa kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB).
Tofauti inayojionesha katika penzi hili ni vile wanaonekana kuwa bize na mambo yao lakini pia kuna muda walijitahidi kufanya siri ikashindikana na kuamua kuendelea kulianika wazi.Pia tofauti na mahusiano yaliyopita ambayo yalikuwa tyakiingiliwa sana na ndugu wa Diamond hasa mama BI Nasra na Esma Platnumz dada yake Diamond Natasha Donna ameonekana kuwa bize na mambo yake na hajawa na muda wa kuwa karibu hata na familia ya Diamond
Wambea wa mambo ya watu maarufu mitandaoni wanadai kwamba kwa sasa imekuwa komesha huku wengi wakimsifu binti huyo kwa kuwachunia watu hao ambao wanaonekana kumwendfesha sana Diamond lakini pia wakisema huyo ndo kiboko yao.
Watu wengine wamekuwa wakipinga vikali uhusiano huo wakiamini ya kwamba ni wakiki na wala hauna maisha marefu kwani imekuwa ni Tabia ya Diamond kujitafutia umaarufu kupitia watu wengine hasa anapotaka kufanya jambo lake(Wakimaanisha tamasha la Wasafi festival lililofanyika nchini Kenya) na wakiamini wala hawezi kumuoa kama anavyojitangaza.
Mambo yamekuwa ni moto na watu wanaendelea kusubiri kuona mwisho wake je itafungwa ndoa ama itakuwa ni hadithi za abunuasi?.Cha kukumbuka ni kwamba ndoa hiyo imepangwa kufanyoika mwaka huu mwanzoni huku hamu kubwa ikiongezeka kujua ni aina gani ya ndoa itafungwa,hadhi yake na mbwembwe ziktakazokuwepo wakijumuisha pia na gharama zitakazotumia.Mambo yanazidi kusogea kikubwa Zaidi tusubiri kuona haya yakitimia lakini yote kwa yote unaambiwa ndoa hiyo itakuwa ni kufuru.

Hata hivyo kupitia Wasafi Tv Diamondametanabaisha kwamba anataka kufanya tukio na kipekee na ambao litahudhuriwa na mastaa kibao ulimwwnguni akiwepo Rick Ross hivyo hatoifanya kwa pupa watu wavumilie.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.