KOCHA MBELGIJI WA SIMBA AMEPANIA AISEE ,AZIPANGA BUNDUKI HIZI HATARI KWENYE MECHI YA KMKM.

Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems ameamua kupanga kikosi Full Masinondo katika mechi ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM, ikielezwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya JS Saoura ya Algeria.

Mashabiki wengi walishangazwa baada ya kikosi cha Simba kuonekana kikiwa sawa na kile ambacho Simba hukitumia kwenye Ligi Kuu Bara.

Sehemu ya benchi la ufundi la Simba limeeleza: “Kocha ameamua kufanya match fitness. Kutaka wachezaji wawe fiti zaidi. Baada ya mechi hiyo wataendelea na mazoezi.

“Lengo ni kujiandaa na Waalgeria halafu pia kuwafurahisha kwa kuwa KMKM ni timu inayoheshimika Zanzibar na mashabiki Simba pia wanataka furaha. Itakuwa mechi ya ushindani na hakuna utani,” kilieleza chanzo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.