KIKUNDI CHA VYAMA VYA SIASA CHAJITOSA KUSAIDIA DAMU HOSPITAL YA NYERERE

Na,Naomi Milton
Serengeti

Kikundi cha ujamaa na ujirani mwema Serengeti (KICHAUMWESE) kinachoundwa na vyama vitano vya siasa kimejitokeza na kuchangia unit 18 za damu kusaidia wahitaji mbalimbali katika Hospitali Teule ya Nyerere ddh

Hospital hiyo bado ina changamoto kubwa ya uhitaji wa damu hasa kwa makundi maalum kama vile mama wajawazito na watoto lakini pia kwa watu majeruhi ambao hupata ajali

Katika mkutano wao mkuu uliofanyika wilayani Serengeti wanakikundi walikabidhi hati ya usajili kwa katibu Tawala wilaya Cosmas Qamara aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na kuahidi kuendeleza umoja wao ambao unalindwa na msingi wa Siasa safi

Mbali na kuchangia damu kikundi hicho pia kimechangia pesa Taslimu shilingi 100,000 katika kuunga jitihada za wilaya za JENGA HOSPITAL KWA SHILINGI 1,000 lengo ni kuhakikisha Hospital ya wilaya inakamilika na kuanza kutoa huduma

Kikundi cha ujamaa na ujirani mwema Serengeti kinaundwa na vyama vya Ccm,Chadema,Cuf ,Nccr Mageuzi na Act Wazalendo kiliundwa mwaka 2015 Kwa ajili ya kusaidia kuimarisha Amani na umoja sasa ni miongoni mwa vikundi vya ujasiriamali vinavyofanya vizuri wilayani hapo

Chimbuko la kikundi hicho ni kwenye vijiwe vya kahawa vya Cheka na wazee na Cheka na vijana ambapo ushabiki ulisaidia kutengeneza kikundi cha kusaidia siasa zisiwe za chuki bali upendo na kuafikiana kuunda umoja wa vyama vya siasa wakiwemo Polisi na makundi mengine hawa saa ni wajasiriamali wanaochipukia kwa kasi kubwa

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.