KIKONGWE AUWAWA KIKATILI NA KUKATWA SEHEMU ZA SIRI

Na Allawi Kaboyo-Bukoba Kagera.

Watu wawili wamepoteza maisha katika mauaji tofauti Mkoani Kagera akiwemo Laurian Kakoto(80)mkazi wa Kijiji cha Ihunga Kata ya Kishanda aliyeuawa na kuzikwa kwa kutanguliza kichwa akiwa amekatwa koromeo na kuondolewa sehemu za siri.

Akifafanua matukio hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Revocatus Malimi amesema tukio la kwanza lilitokea mnamo tarehe 08/01/2019 linahusishwa na imaani za ushirikina ambapo mwili wa marehemu Kakoto ulikutwa umefukiwa kwenye shimo la mita moja kwenye shamba la mahindi.

Kamanda Malimi amesema marehemu aliondoka nyumbani kwake tarehe 7,Januari,2019 kwenda kununua mchele na unga ambapo kando ya shimo ulipofukiwa mwili wa marehemu umekutwa mfuko wa mchele na msako dhidi ya watuhumiwa unaendelea.

Pia katika tukio jingine nyumba kumi na sita zimeteketezwa kwa moto Wilayani Kyerwa katika kijiji cha Kibingo baada ya mwili wa mwendesha bodaboda Albert Antipas aliyetoweka tangu tarehe 2,Januari,2019 kugundulika kwenye bwawa la kufugia samaki.

Kamanda Malimi amesema baada ya kuonekana kwa mwili huo wananchi zaidi ya 300 walihamasishana wakiwa na silaha za jadi na kuchoma nyumba na kufyeka migomba kwa watu waliodhaniwa kuhusika na mauaji hayo.

Amesema watuhumiwa watatu wanashikiliwa na Polisi baada ya kukutwa na pikipiki MC 151 CAM aina ya KINGLION aliyokuwa akiendesha marehemu ambapo watu wawili wamejeruhiwa kwa kukatwa mapanga katika vurugu hizo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.