KIASI CHA SHILINGI BILIONI 12 ZAHITAJIKA KUHAMISHA MAGEREZA IRINGA MJINI

kamishina jenerali wa magereza nchini Phaustine Kasike akiwasili mkoani Iringa kikazi

Na Francis Godwin,Iringa

KIASI  cha  shilingi  bilioni 12 zinahitajika kwa  ajili ya  kuhamisha  gereza  la Iringa mjini  ili  kupisha  upanuzi wa hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa .
Kamishina jenerali  wa  magereza  nchini  Phaustine  Kasike   hayo leo   wakati wa  ziara  yake  mkoani Iringa na  kuwa  tayari  mchakato wa  kuhamisha  gereza  hilo  umeanza  katika eneo la mlolo  nje ya  Manispaa ya  Iringa .
Kasike  alisema  kuwa  hivi  sasa  maandalizi ya  ujenzi wa nyumba  za  watumishi  wa magereza  yanafanyika katika  eneo la  Mlolo  na  tayari  baadhi ya  vifaa vya  ujenzi kama  mawe na  matofali  yamekwisha  tayarishwa  na   kazi nyingine  zinaendelea.
”  Suala  la uhamishia  wa  gereza  la  Manispaa ya  Iringa   serikali  tayari  ilikwisha  toa maelekezo   kuwa  gereza hilo  liweze  kuhamisha  na  sisi  pia  tunafahamu  kuwa  gereza   linahitaji  kuwa na eneo  kubwa  zaidi  ili  tuweze  kufanya kazi  zetu  kwa  ufanisi zaidi  na  pasipo  kuingiliwa na raia wengine    ni kweli  hatuwezi kufanya   kazi  zetu  kifanisi   hivyo  tayari  tumeanza  kuandaa  eneo la  ujenzi  katika ardhi  yetu  yenye  ukubwa wa  zaidi ya  hekari 812 ” alisema   Kasike
Kuwa  eneo  hilo litajengwa  nyumba  za  watumishi  pamoja  na   gereza  kubwa la  kisasa  ,viwanja  vya  michezo  na litatumika kuendesha  shughuli  mbali mbali  za  uzalishaji  mali kama  kilimo na nyingine  ili  kuweza  kujiendesha .
Alisema  kuwa  kwa  kuwa  changamoto  ni   upatikanaji  wa  fedha    za  ujenzi  wa gereza  mpya  ila  wao kama  magereza  wanaendelea  kutumia  raslimali walizonazo  kuendelea na maandalizi ya  ujenzi wa  gereza  hilo  ambalo pia  litapunguza  msongamano wa  wafungwa  katika  magereza  ya  Iringa .
Kwani  alisema  mpango  wao  kujenga  gereza   kubwa  zaidi  ambalo  litahifadhi  wafungwa  zaidi ya  1000 wa  makundi  mbali mbali    kwani kwa  eneo  walilonalo ni  kubwa  zaidi .
Kuhusu  utekelezaji  wa agizo la  Rais Dkt  John Magufuli  la  magereza  kujikita katika  uzalishaji   ,Kamishina  Kasike  alisema  tayari  amekwisha  fanya  ziara  katika  mikoa mbali mbali  ya  Tanzania  na anaendelea  kufanya  ziara  ikiwa ni  pamoja na  kutenga magereza  ambayo yatatumika  kwa  ajili ya uzalishaji wa mazao ya  chakula  kwa  ajili ya  kuhudumia  magereza  mengine .
Alisema kwa mkoa wa Iringa  eneo la Pawaga  lina ardhi  kubwa ambayo inafaa kwa uzalishaji wa mazao  mbali mbali kama mpunga ,mahindi  na mazao  mengine pia  gereza la Isupilo  wilayani  Mufindi lina eneo  kubwa la uzalishaji pamoja na gereza la Kihesa  Mgagao  wilaya ya  Kilolo .
Kwa  upande  wake mwakilishi  wa mkuu wa mkoa wa Iringa katika kikao  hicho mkuu wa  wilaya ya  Iringa Richard Kasesela  pamoja na  kupongeza mipango ya kamishina  huyo wa magereza kwa  ajili ya uhamishaji wa  gereza la Iringa bado  alimwomba  kufika  kujifunza  katika  kiwanda  cha Maziwa cha  Asas Dairies Ltd ili  kuona  wao kama  magereza  kupitia ufugaji wa ng’ombe watakavyoweza  kuwa washiriki  wa kiwanda  hicho kwa uuzaji  wa  maziwa  yanayozalishwa na magereza.
Pia  Kasesela  alisema  suala la  kuhamishwa  kwa  gereza  la Iringa ni  kilio  kikubwa kwa  Iringa hasa  ukizingatia  ufinyu na  gereza  la sasa na  msongamano wa  wafungwa hivyo hatua ya  kuhamishwa kwa  gereza  hilo  ni  nzuri  ila   itasaidia  pia  upanuzi wa  hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa .
Askari Magereza Iringa wakimsikiliza kamishina jenerali wa magereza nchini Phaustine Kasike (hayupo pichani )
ACP Hasserd Mkwanda mkuu wa magereza Iringa akimkaribisha kamishina jenerali wa magereza nchini kuzungumza na askari
Mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Iringa Richard Kasesela akimpokea kamishina jenerali wa magereza nchini Phaustine Kasike alipofika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kusaini kitabu cha wageni leo
kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire akijiandaa kusalimiana na kamishina jenerali wa magereza nchini Phaustine Kasike leo

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.