KATIBU MKUU WA CCM AONGOZA UJUMBE ZIARA YA KIMKAKATI NCHINI CHINA

Ujumbe wa Viongozi wa CCM umeondoka leo kuelekea nchini China kwa ziara ya kimkakati inayolenga kuongeza mahusiano kati ya CCM na Chama Cha Kikomunisti cha Watu wa China (CPC), Kamaradi Bashiru Ally Katibu Mkuu wa CCM anaongoza ujumbe huo.

Akizungumza kabla ya kuanza safari Kamaradi Bashiru ameelezea safari hiyo kwamba ni ya kimkakati na inalenga kuimarisha mahusiano kati ya CCM na CPC. Aidha amesisitiza safari hiyo pamoja na mambo mengine ujumbe wa viongozi hao utakwenda kubadilisha uelewa, uzoefu na kujifunza mikakati ya kujitegemea kirasilimali ili kuendesha Chama, namna bora na bunifu ya kuendesha Miji na Majiji nchini na namna bora ya kujenga mahusiano kati ya Chama na Serikali katika kutoa maendeleo kwa watu.

Ujumbe wa Chama Cha Mapinduzi umejumuisha kwa uwakilishi viongozi wa Chama Taifa ikiwamo wajumbe wa Baraza la Wadhamini, Jumuia za Chama, Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Wajumbe wa Bodi za Kampuni za Chama na Maafisa wa Chama kutoka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu. Chama Cha Mapinduzi katika ujumbe huu kimejumuisha maafisa wawili wa Serikali ili nao wakajifunze kama sehemu ya ujumbe huo.

Ujumbe wa CCM utakuwa Nchini China kwa siku 10 na utakuwa na fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali wakiangazia fursa za mashirikiano na uwekezaji kwa maslahi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Taifa.

Wakati uo huo Kamaradi Bashiru ametumia nafasi hiyo kuwashukuru kwa dhati watanzania wakaazi wa Wilaya ya Liwale na Jimbo la Liwale kwa uchaguzi mzuri uliokamilika kwa Amani na usalama na kukiwa na idadi kubwa ya wananchi waliojitokeza kupiga kura ambapo Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mgombea wake Zuberi Kuchauka kimeibuka na ushindi wa kishindo.

Huu ni muendelezo wa mikakati ya kukuza mahusiano ya kimataifa, diplomasia ya siasa na uchumi kwa manufaa ya nchi yetu Tanzania.

Imeandaliwa na Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa na Idara ya Itikadi na Uenezi na,

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.