KAMPUNI YA GREEN MILES YAAGIZWA KUINGIA MIKATABA NA VIJIJI VILIVYOPO KWENYE KITALU CHAKE.

Longido,Arusha.

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Longido limeaiagiza kampuni ya uwindaji ya Green Miles kuingia mikataba na wananchi waliopo katika vijiji vilivyopo katika kitalu chake.

Maagizo hayo yametolewa 13 September 2018,wakati wa kikao cha kawaida cha madiwani hao.

Baraza hilo la madiwani chini ya mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Sabore Molloimet na mkurugenzi mtendaji, Jumaa Mhina,limepokea Taarifa za Kamati za kudumu za halmashauri fedha,utawala na mipango, kamati ya elimu, afya na maji, Kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira na Kamati ya kudhibiti Ukimwi ambapo masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo mgogoro wa kisheria kati ya mwekezaji wa kampuni ya Green Miles Safari Ltd, Halmashauri,
na vijiji 23 vilivyo kwenye Kitalu kinachosimamiwa na kampuni hiyo.

Mgogoro huo umetokana na kampuni hiyo kushindwa kulipa ushuru wa huduma kwa Halmashauri,kushindwa kuvilipa vijiji 23, kufanya doria za kukabiliana na uwindaji haramu kwenye kitalu chake na mahusiano mabaya na jamii.

Baada ya majadiliano baraza limeazimia mwekezaji huyo alipe madeni anayodaiwa na kuingia mikataba na vijiji vyote anavyostahili kuvilipa,pamoja na kuweka mpango wa kufanya doria shirikishi.

Pia imeamriwa kuwa zuio la Halmashauri kutoa wataalam wake kuwida kwenye kampuni hiyo litaondolewa baada ya mikataba ya kisheria kusainiwa baina ya kampuni na vijiji ifikapo 20 september 2018.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Longido mh.Frank Mwaisumbe amesema hatamvumilia yeyote atakayemnyima mwananchi mnyonge haki yake au atakayekwepa kulipa kodi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.