KAMPENI YA FURAHA YANGU WILAYANI NAMTUMBO YAZIDI KUCHANJA MBUGA.

 

 

Namtumbo

Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo mheshimiwa Sophia Mfaume ameendelea na kampeni ya furaha yangu kwa kufungua mashindano ya mpira wa miguu wilayani humo.

Aidha amesema kuwa, wilaya hiyo,wameendeleza jitihada zao kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu iitwayo Laiganani super cup ambapo maana ya jina hilo ni neno la kimasai linalohamasisha vijana.

“Tumeendeleza jitihada hizi kwa kuanzisha ligi ya mpira wa miguu ambapo lengo ikiwa ni kuhamasisha vijana kujitokeza kupima, kujitambua afya zao na watakaokutwa na VVU kuanza dozi mapema ” amesema DC Kizigo

Aidha amesema, lengo kuu la kuongeza kiwango cha upimaji wa VVU hasa kwa wanaume hadi juzi tarehe 18/10/2018 wilaya ya Namtumbo walipima wanaume 873 na 16 walipatikana na VVU ambao kati yao 13 wameshaanza dozi (ARVs).

Katika kupambana na UKIMWI na kujenga jamii yenye uelewa na furaha, Serikali ilianzisha kampeni ya Furaha yangu iliyozinduliwa na mheshimiwa Waziri Mkuu kitaifa na kwa Mkoa wa Ruvuma ilizinduliwa na Waziri wa Afya mhe. Ummy Mwalimu tarehe 31/8/2018.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.