JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAKABILIWA NA KITISHO CHA UGONJWA WA EBOLA

 

 

Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Uganda, Sudan Kusini, Rwanda na Burundi zimetakiwa kuchukua tahadhari ya haraka kutokana na kusambaa kwa ugonjwa wa Ebola, kwa sababu hali inaweza kubadilika wakati wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani (WHO).

WHO linasema hatari ni kubwa kwa Uganda, Rwanda, Burundi na Sudan Kusini na tayari nchi hizo zimeambiwa kuchukua hatua za haraka ili kuzuia ugonjwa huo.

Kauli hii inakuja baada ya mkutano maalumu wa dharura uliofanyika mjini Geneva kujadili hali ya ugonjwa huu nchini DRC.

Burundi na Sudan kusini ni nchi mbili za Afrika Mashariki ambazo zinaonekana kuwa katika hatari zaidi kutokana na kuingia na kutoka kwa watu mpakani kutoka nchi za DRC, Rwanda na Uganda.

Wizara ya afya nchini Burundi imeeleza kwamba tayari kuna vifaa vya kukabiliana na janga iwapo litatokea.

Shirika la afya (WHO) limesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC bado hauhitaji jitihada za dharura za kimataifa huku likisisitiza kuwa linafuatilia kwa karibu ugonjwa huo.

Kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na mzozo unaoendelea, Kupoteza imani kwa jamii katika maeneo yalioathirika, yote haya yanatatiza jitihada za kudhibiti ugonjwa huo.

Takwimu kutokana na mlipuko uliopo sasa wa Ebola nchini DR, unaonyesha kwamba kati ya watu 10 walioambukizwa Ebola 6 hufariki.

Mapigano katika eneo hilo yanafanya kuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo.

Kwa sasa tahadhari imetolewa kwa wananchi kutosafiri kwenda katika maeneo yalioathirika na kuripoti dalili zozote wanazozishuku.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.