JKT-TANZANIA” TUNAOMBA TFF WACHUKUE HATUA DHIDI YA MWAMUZI MBARAKA RASHID.”

Na Prakseda Mbulu,
Mbeya.

Uongozi wa timu ya soka inayoshiriki ligi kuu Tanzania Bara JKT-Tanzania imeitaka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF,kumchukulia hatua mwamuzi aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Simba SC,Mbaraka Rashid,kwani mechi hiyo ilikuwa na kasoro nyingi.

Akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa kumbukumbu ya sokoine Jijini Mbeya,Afisa habari wa Club hiyo Jamila Mutabazi amesema kwa ujumla michezo ule uliochezewa katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga November 3,2018 haukuwa sawa kwani mwamuzi alionekana wazi kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu kutokana na kuyaacha makosa ya wazi waliyoyafanya wachezaji wa timu ya simba uwanjani.

“Kwa mfano Kuna baadhi ya matukio ambayo hatukuridhika nayo,mchezaji wa Simba alishika mpira kwa mkono mara ya kwanza na ikajirudia mara ya pili lakini mwamuzi hakutaka kutupa penalty”amesema Mutabazi.

“Kwa ujumla tulitakiwa kupewa penalty mbili za wazi,hivyo tumeona mwamuzi hakututendea haki hali iliyopelekea kutoa kadi nyekundu kwa mchezaji wetu Ally Ahmed maarufu kama Shiboli,hii inaonesha mwamuzi alikuwa na masilahi yake binafsi ama alikuwa na ushabiki.” ameongeza Mutabazi.

Mutabazi amesema kupitia hilo,wameliandikia barua ya malalamiko shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF,ili kuangalia baadhi ya waamuzi wanaochezesha mpira,kwani wengi wanonekana kuwa na ushabiki wa timu wanazokuwa wanachezesha hali inayowafanya washindwe kuzuia hisia zao.

“Kwa kuwa michezo ulikuwa live tunavithibitisho vyote kwa kile kilichotokea uwanjani na tunavipeleka mahali husika ili sheria ichukuliwe na ilete maana kwa baadhi ya waamuzi ambao sio waadilifu katika majukumu yao.”Amesema Mutabazi.

Aidha kuhusu mchezo wao dhidi ya timu ya Mbeya City November 8 mwaka huu,amesema kuwa wanajua timu ya Mbeya city ipo vizuri lakini wanaimani watafanya vizuri kwani wachezaji wao wamenolewa vizuri na mwalimu wa timu hiyo.

Timu ya JKT-Tanzania inakutana na Mbeya city ikiwa ni mchezo wao wa 124,katika dimba la Sokoin jijini Mbeya huku ikiwa nafasi ya saba,sawa na Mbeya city ambayo wamezidiana idadi ya magoli.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.