JESHI LA POLISI LINAMSHIKILIA MBUNGE BWEGE NA VIONGOZI WA CUF KILWA

Kilwa

Katibu Itikadi na Uenezi wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Sheibu, amesema amepokea taarifa hivi punde kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini Seleman Bungara (Maarufu kwenye ulingo wa siasa kwa jina la Bwege) amekamatwa na Polisi huko Jimboni kwake Kilwa.

Aidha amesema licha ya Mbunge huyo, pia wamekamatwa madiwani watano wa CUF, Katibu wa Mbunge, Deo Chaurembo, Mkurugenzi wa siasa wa CUF Kilwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilwa.

Katika taarifa iliyotolewa na kiongozi huyo, imeeleza kuwa, madai ya Jeshi la polisi ni kwamba, Bwege hakutoa taarifa ya mkutano wake kwa polisi ambapo kabla ya kuvamia mkutano huo, kutawanya wananchi kwa mabomu na kuwakamata viongozi hao, Katibu wa Mbunge aliwaonesha Polisi nakala ya barua iliyowasilishwa kwa kwao, lakini hawakujali walieendelea kuwakamata.

Kutokana na tukio hilo, amesema hivi karibuni amekaririwa na vyombo vya habari, Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola akitoa kauli ya kulionya Jeshi la Polisi kujiepusha na vitendo vya kuwakamata watu na kuwaweka ndani, kiholela.

“Swali langu kwa Waziri wa Waziri wa Mambo ya Ndani hivi karibuni umekaririwa na vyombo vya habari ukitoa kauli za kulinyoosha Jeshi la Polisi kwenye jambo hili ama lile kiasi cha kuwakuna baadhi ya watetezi wa haki za binadamu na wapenzi wa haki kote nchini ” amesema Ado.

Ameendelea “Mbona matendo ya jeshi la polisi yanaendelea kutosadifu maelekezo na matamko yako? Kwa nini Jeshi la Polisi linaendelea kuwabughudhi wabunge wa upinzani kutekeleza wajibu wao? Tafadhali welekeze OCD Kilwa aache kazi ya siasa kwa wanasiasa na amwachie huru Bwege mara moja”amehoji Ado.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.