JENERALI JESHI LA MAREKANI AKIRI KUSHINDWA KUIDHIBITI TALIBAN HUKO AFGHANSTAN.

 

Kabul, AFGHANSTAN.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Marekani, upande wa Mashariki ya Kati, Luteni Jenerali Kenneth McKenzie, amekiri kuwa vita vya Afghanistan vimeishia kwenye mkwamo na kupelekea maafa makubwa ya roho za raia wa nchi hiyo, maafa ambayo hayawezi kuvumilika.

Awali Bw Joseph Dunford, ambaye ni Mkuu wa vikosi vyote vya ulinzi vya Marekani naye alikiri kuwa, kundi la Taliban haliwezi kushindwa wa vita vya Afghanstan na kwamba utumiaji nguvu za kijeshi kwa ajili ya kuhitimisha vita nchini humo umegonga mwamba.

Baadhi ya maafisa, wabunge, shakhsia wa kisiasa na kidini, pamoja na wataalamu wa masuala ya Afghanistan, wamesisitiza mara kadhaa kuwa, Marekani imeshindwa kudhamini usalama na kuhitimisha vita nchini Afghanistan, hivyo inapaswa kuondoa majeshi yake katika ardhi ya nchi hiyo.

Kwa mtazamo wa viongozi na wananchi walio wengi wa Afghanistan, taifa hilo kuwepo kijeshi nchini Afghanistan tangu mwaka 2001 kwa kushirikiana na nchi nyingine wanachama wa shirika la kijeshi la NATO, kumekuwa kama kisingizio cha kupambana na ugaidi, Jambo ambalo halijazaa matunda wala kupata mafanikio yoyote zaidi ya kuongeza idadi ya vifo katika pande zinazopigana, kuua maelfu ya raia wasio na hatia na kuteketeza miundombinu ya nchi hiyo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.