JE UNAFAHAMU KUWA MAREKANI INAVYO VITUO VYA KIJESHI ZAIDI YA 30 VYA SIRI BARANI AFRIKA?

 

New York, MAREKANI.

Tovuti moja ya habari ijulikanayo kama Intercept iliyopo jijini New York nchini Marekani, imefichua habari za kuwepo kambi za kijeshi za siri za nchi hiyo zilizopo katika nchi kadhaa barani Afrika.

Tovuti hiyo imefichua nyaraka za siri kuhusu kambi hizo za kijeshi za Marekani barani Afrika kwa kutumia Sheria ya Uhuru wa Habari.

Nyaraka hizo zimemnukuu Peter E. Teil, Mshauri wa Masuala ya Sayansi wa Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani Afrika (Africom) akisema kuwa, kuna vituo 34 vya kijeshi ambavyo havijatangazwa hadharani au kuwekwa wazi na serikali ya Washington katika nchi za Somalia, Libya na Niger.

Aidha, tovuti hiyo ya Intercept pia imemnukuu bw Adam Moore, Naibu Mhadhiri wa somo la Jografia katika Chuo Kikuu cha California nchini Marekani akisema kuwa, ni ajabu kwa Marekani kudai kuwa uwepo wake wa kijeshi barani Afrika ni mdogo, ilihali ina vituo vya siri na dhahiri katika nchi za Somalia, Djibouti, Kenya, Libya, na katika nchi za eneo la Sahel (yaani Cameroon, Chad, Niger, Mali, na Burkina Faso).

Bw Moore ameashiria pia hatua ya Washington ya kujenga kituo cha ndege zisizo na rubani (drone) za kijeshi nchini Niger kwa shabaha eti ya kukabiliana na makundi ya kigaidi.

Kituo hicho cha drone kinachojengwa katika mji wa Agadez nchini Niger ni moja vya vituo vikubwa zaidi kuwahi kujengwa na Marekani katika nchi ajinabi.

Marekani inaendelea kupanua ujasusi wake na kujenga vituo vya kijeshi katika nchi za Afrika kwa visingizo mbalimbali.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.