JAMII YATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUIBUA MATUKIO YA UKATILI DHIDI YA WATOTO.

Dodoma.

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto,imewataka wazazi,walezi na jamii kwa ujumla kuzingatia ulinzi wa mtoto ili kutekeleza lengo la la kupunguza matukio ya ukatili kwa silimia 50 ifikapo mwaka 2021!2022.

Aidha,wizara hiyo imeitaka jamii kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii kwa kuepuka kutuma picha za watoto ambao ni wahanga wa ukatili na kuziweka wazi kinyume cha sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

Taarifa ya wizara imetolewa leo,baada ya kuwepo kwa taarifa mapema wiki hii juu ya mwalimu mmoja wa shule ya msingi jijini Dodoma,kumfungia mtoto ndani ya kabati kwa kipindi kirefu na kusababisha afya ya mtoto huyo kudhoofika ambapo imelaani na kukemea vikali vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoendelea kujitokeza nchini.

Wizara hiyo imesema,vitendo hivyo vinafanywa kwa kuhusisha ndugu na walezi wa karibu wa watoto hivyo kuzua hofu kubwa kwa watoto na jamii na hatimaye kuathiri makuzi ya awali ya watoto kutokana na kutozingatia haki zao za msingi.

Imesema vitendo vya ukatili vinapotokea majumbani,vinarudisha nyuma jitihada za serikali za kulinda na kuendeleza haki na ustawi wa watoto katika ngazi ya familia ambayo ni kitovu cha jamii wakiwemo watoto.

Pia Wizara hiyo imeipongeza jamii na wote walioibua tukio hilo na hatimaye kuwezesha jeshi la polisi kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ua uchunguzi ili sheria ichukue mkondo wake na hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa, na kuomba utulivu na uvumilivu ili kutoa nafasi kwa vyombo vya dola kufanya uchunguzi kwa umakini.

Hata hivyo ametoa pole kwa wazazi,ndugu na marafiki wa familia ya mtoto aliyefanyiwa ukatili huo huku ikiomba ushirikiano na jamii katika kufichua vitendo vyote vya ukatili dhidi ya watoto vinavyojitokeza katika maeneo yao.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.