IDADI YA VIFO KUTOKANA NA MAFURIKO YAONGEZEKA JAPAN

Nchini Japani idadi ya vifo kutokana na mafuriko imeongezeka mpaka kufikia 109. Watu wengine 80 bado hawajulikani walipo mpaka hivi sasa huku maelfu ya watu wakiwa wamelazimika kuyahama makazi yao.

Haya mafuriko na maporomoko yametokea katika maeneo 19 tofauti nchini humo, na eneo hasa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni eneo la Hiroshima .

Waathirika wengine wameripotiwa katika maeneo ya Ehime, Okayama, Yamaguchi, Kyoto, Gifu, Shiga, Hyogo, Kochi na Fukuoka.

Zoezi la uokoaji bado linaendelea katika ameneo hayo.
Mamlaka imetangaza kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka kutokana na kunaswa kwa baadhi ya watu katika majumba yao.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.