HICHI NDICHO ALICHOKISEMA OMMY DIMPOZ KWENYE SIKU YAKE YA KUZALIWA

 

 

Msanii maarufu nchini wa muziki wa bongo fleva, Ommy Dimpoz kupitia ukurasa wake wa instargram amesema namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjalia kuuona mwaka mwingine licha ya majaribu mengi alioyapitia kwa kipindi cha miezi mitano iliopita.

“Leo 13th September ni kumbukumbu yangu ya siku ya kuzaliwa.
Namshukuru sana Mwenyezi Mungu (ALHAMDULILAAH) kwa kunipa nafasi ya kuuona mwaka mwingine, kwani niliyoyapitia katika kipindi cha takribani miezi 5 kama ingekuwa sio mapenzi yake yeye (M/Mungu) basi ingekuwa imebaki history” – Ommy Dimpoz

Ameseam kuwa, alichojifunza kipindi hicho chote ni kuwa kuumwa ni Ibada na sisi kama binadamu hatujakamilika leo unaweza kuwa mzima na kesho ukawa mahututi kitandani, ndio maana nimeamua kushare picha ambayo nilipigwa nikiwa ICU japo nafahamu sio kitu kizuri kupost picha kama hii kwenye mitandao ila nia yangu ni kujaribu kukumbushana sisi kama Binadamu kuwa kuna leo na kesho kwahiyo tusiishi kwa chuki na Uadui maana hatujui kesho yetu itakuwaje.

“Kuna kipindi wakati nimelazwa nilikata tamaa ya kuishi nikaona labda muda wangu umekwisha lakini hapo Hospital akaletwa mgonjwa mwingine ambae alikuwa pembeni yangu alishambuliwa na majambazi kwa risasi tisa mwilini lakini madaktari wakafanikiwa kuokoa maisha yake na akapona so nikajiuliza mimi ni nani nikate tamaa ya kuishi na nikajifunza kwamba kuugua sio kufa” – Ommy Dimpoz

Aidha amesema, ni vyema tukipata nafasi basi tuwaombee na kuwafariji wagonjwa kwani wanayoyapitia ni magumu mno, na tukielewa maisha ni mapito tu.

“Kwasasa namshukuru Mwenyezi Mungu naendelea vizuri na bado niko kwenye recovering, pia nawashukuru watu wote ambao mmekuwa mkiniombea dua nipone kwa haraka kuanzia mashabiki mpaka wasanii wenzangu na kila mtu aliyeniombea kwa imani yake Nashukuru sana. Mungu awabariki sana” – Ommy Dimpoz

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.