HAMAS YAOMBA AFRIKA KUSINI KUINGILIA KATI KUSAIDIA MAPAMBANO YA UKOMBOZI WA WAPALESTINA.

 

Pretoria, AFRIKA KUSINI.

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeiomba Afrika Kusini izidishe uungaji mkono na misaada yake kwa taifa la Palestina katika mapambano yake ya ukombozi dhidi ya utawala haramu wa Israel.

Wito huo umetolewa na ujumbe wa Hamas ulioko nchini Afrika Kusini kwa shabaha ya kupata uungaji mkono zaidi wa Pretoria kwa mapambano ya ukombozi ya Palestina.

Katika mazungumzo yake na Spika wa Bunge la Afrika Kusini mjini Pretoria, ujumbe wa Hamas unaoongozwa na Mahmoud al Zahhar umepongeza hatua zinazochukuliwa na bunge la nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na mipango yake ya kutaka kupunguza uwakilishi wa kidiplomasia na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwawezesha Wapalestina kuingia nchini humo kirahisi.

Ujumbe wa Hamas nchini Afrika Kusini pia umezitaka jamii za Waislamu katika nchi mbalimbali kuelimisha jamii kuhusu mapambano ya ukombozi ya watu wa Palestina dhidi ya Wazayuni maghasibu, kutetea haki zao na kuzihimiza serikali na tawala zao kuunga mkono mapambano ya Wapalestina

Katika mazungumzo hayo kiongozi wa chama tawala cha ANC katika bunge la Afrika Kusini, Jackson Mthembu, amesisitiza kuwa, serikali ya Pretoria itaendelea kulitetea taifa la Palestina na kuunga mkono mapambano yake ya kupigania uhuru.

Aidha, Bw Mthembu amesisitiza kuwa, chama cha ANC kinapinga hatua zinazochukuliwa na Israel dhidi ya taifa la Palestina na kusisitiza kuwa, Afrika kusini inachunguza hatua ya kupunguza uwakilishi wake wa kidiplomasia na Israel hadi kufikia kiwango cha kukata kikamilifu uhusiano wake na utawala huo mbovu.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.