HALMASHAURI ZA WILAYA KOTE NCHINI ZIMEAGIZWA KUTENGA FEDHA KUTOKA MAPATO YA NDANI,KWA KUSHIRIKIANA NA WANAINCHI KUJENGA NYUMBA ZA WATUMISHI WA JESHI LA POLISI.

MULEBA, KAGERA.
Na Mwandishi wetu.

Waziri wa mambo ya ndani Kangi Lugola ametoa agizo hilo jana Januari 8,2019 kwenye mkutano wa hadhara, uliofanyika uwanja wa Fatuma Muleba mjini mkoani Kagera na kwamba nyumba hizo zijengwe palipo na kituo cha polisi

Lugola amesema askari wanatakiwa kuishi kambini kwenye makazi ya pamoja na kulinda maadiliyao ya kiutendaji wakiwa na familia zao badala ya kuishi mitaani na kukiuka misingi ya utumishi wa Umma na wengine kushawishiwa na rushwa

Amesema halmashauri nyingi nchini kwa kutumia kamati za ulinzi na usalama zikijipanga zitaweza kuanzisha maboma ya nyumba za polisi kama zinazvyojengwa nyumba za walimu wahudumu katika sekta ya afya na idara nyingine

‚ÄúAskari anahitaji mazingira tulivu hata kama hana familia, badala ya kutoka kazini amechoka na kuhangaishwa akidaiwa pango wakati huohuo likitokea tatizo la usalama yeye ndiye kichokoo cha kukabiliana na mapambano‚ÄĚ Amesema Lugola

Aidha amesema iwapo halmashauri zitaonesha juhudi za kujenga nyumba za askari kwa kushirikisha wananchi serikali itajitahidi kutoa mahitaji ya viwandani kama mabati saruji na mengineyo kuwamotisha wafanye kazi kwa uadilifu zaidi.

Pia Waziri Lugola ameagiza kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kagera Revocatus Malimi ndani ya siku saba, kusaka wanume wanaotuhumiwa kuwasababishia ujauzito wanafunzi wa shule za msingi na sekondari na kuwafikisha mahakamani

Mkuu wa wilaya ya Muleba Richard Ruyango akitoa taarifa ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, amesema polisi wameisaidia wilaya kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu, ujangili wa wanyama hifadhi za Burigi na ranchi za Taifa mkoani Kagera.

‚ÄúVijana wanawajibika kiuzalendo kulitumikia taifa lao kuwalinda wananchi, huko visiwani hakuna nyumba za kudumu hivyo kuhatarisha usalama wao hata miundombinu ya usafiri kuwahi matukio ya uhalifu ni tatizo‚ÄĚ Amesema Ruyango .

Amesema pamoja na kupongeza askari polisi, bado wanaishi mazingira magumu kiutendaji kwa kuishi nyumba moja na raia lakini wanateseka hasa walioko vituo vidogo vya polisi visiwani ndani ya ziwa viktoria.

Katika mkutano wa waziri Lugola, waanchi wamelalamikia baadhi ya askari polisi kwa kuwabambikizia kesi huku madereva wa magari wakilalamikia tabia ya askari wa usalama barabarani kuwapiga tochi wakiwa wamejificha vichakani.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.