HALMASHAURI YA RUANGWA YAMWAGA MIKOPO KWA WALEMAVU NA WANAWAKE.

Na Bakari Chijumba,Lindi.

Vijana,wanawake na walemavu wilayani Ruangwa mkoani Lindi, wamewezeshwa na halmshauri kwa kupatiwa mikopo ya vikundi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Kupitia mikutano ya hadhara iliyofanyika kwenye vijiji vitano, 04 Disemba 2018, wakati wa ziara ya mkuu wilaya kwenye kata ya Nandagala wilayani humo, wanufaika wa mikopo hiyo wameushukuru uongozi wa halmashauri na kuutaka uendeleze utaratibu huo wa kutoa mikopo kwa vikundi vingi zaidi.

Saidi Omari mkazi wa kijiji cha Mmawa, amemshukuru na kumpongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Ruangwa, Andrew Chezue, kwa mikopo hiyo anayowapatia kupitia idara ya maendeleo ya jamii na kusema inawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuendesha familia.

“Tusiposhukuru tutakuwa wachoyo wa fadhira, kwani mkurugenzi wa awamu hii anatimiza wajibu wake ipasavyo na mikopo tunaipata kama inavyotakiwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma” amesema Saidi .

Naye Hawa Napeya mkazi wa Namaheba B, amesema mikopo wanayopata inawasaidia sana na amewaomba wakazi wa Ruangwa wanaonufaika na mikopo hiyo waitumie kwa malengo waliojiwekea ili iwe rahisi katika kurudisha kwa wakati.

“Fedha tunazokopeshwa tunapaswa kuzirudisha ili na wengine waweze kupatiwa tujitahidi kuzipangia malengo ya kudumu ili tuwasaidie na wengine kupata mikopo kama ambavyo sisi tunapata” amesema Hawa.

Wananchi hao kwa pamoja wamesisitiza na kuendelea kuiomba Halmashauri hiyo, iendele kutoa mikopo kwa vikundi ambavyo havijapata, ili kuepusha wimbi la vijana wasio na ajira mtaani.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.