GABRIEL JESUS AFUNIKA UEFA CHAMPIONS LEAGUE

Na Shaaban Rwapi.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City, Gabriel Jusus usiku wa jana ulikuwa mzuri kwake kwenye mchezo wa Uefa Champions League baada ya kufunga Hat-trick kwenye ushindi wa 6 – 0 huku magoli mawili akifunga kwa penati dhidi ya Shakhtar Donetsk

Jusus anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga penati mbili kwenye mchezo mmoja kwenye michuano ya Uefa Champions League kwa timu kutoka Uingereza, toka mwaka 2011 Mshambuliaji Wayne Rooney akiwa na Manchester United kufanya ivyo kwenye mchezo dhidi ya Otelul Galati.

Pia Jusus anakuwa katika list ya wacheza wa tatu wa Manchester City kufunga hat-trick kwenye michuano ya Uefa Champions League baada ya
Sergio Kun Aguero kufanya ivyo mara mbili na mchezaji Alvaro Negredo mara moja.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.