FAHAMU UMUHIMU WA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU.

 

Tangawizi ni nini?

Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake.

Pia  bidhaa hii inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia.

Zifahamu faida/umuhimu wa Tangawizi.

 • Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wanawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika.
 • Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia maumivu makali kupata ahueni, pia husaidia kusambaza damu kwenye mwili kwa haraka zaidi.
 • Husaida msago wa chakula kwa haraka zaidi kwa kuchanganya na tindikali tumboni.
 • Husaidia kwa wale wanaosafiri baharini ikiwa na machafuko kuzuia kutapika,kwa kutumia nusu saa kabla ya kusafiri na boti.
 • Husaidi kupigana na kukinga kansaa ya kizazi.
 • Tangawizi husaidia kupunguza maumivu mwilini.
 • Wataalamu wamegundua tangawizi ni dawa tosha ya presha kuliko kitunguu swaumu.
 • Husaidi kuponya fluu kwani chai ya tangawizi ni salama
 • Tangawizi inatumika kutuliza maumivu ya tumbo, yanayotokana na matatizo ya
  usagaji chakula, kuharisha, kuvimbiwa, n.k. Inapotumiwa katika chakula tangawizi husaidia usagaji chakula.
 • Matatizo ya Moyo: Tangawizi huimarisha moyo wa binadamu na kumwepushia maradhi ya moyo. Hii ni kwa kuwa inapunguza kiwango cha mafuta mwilini.
 • Huondoa homa ya mafua, hutumika kutibu pumu, na pia kufungua mfumo wa upumuaji hasa inapotumika pamoja na asali.
 • Huondoa maumivu ya misuli, kichwa, na shinikizo la mawazo, kisunzi, na kukosa umakini.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.