DOS SANTOS KUONDOKA RASMI KATIKA SIASA ZA ANGOLA JUMAMOSI IJAYO

Luanda, ANGOLA.

Rais wa zamani wa Angola, Jose Eduardo dos Santos, anatarajia kustaafu moja kwa moja katika ukumbi wa siasa mwishoni mwa wiki hii na kukabidhi uongozi wa chama tawala kwa mrithi wake Rais wa nchi hiyo Joao Lourenço.

Dos Santos ambaye ni mgonjwa kwa sasa, alianza kutawala Angola mnamo mwaka 1979 na aliomba kuachia ngazi kwa amani, kinyume na wenzake wengi wa Afrika.

Mwaka mmoja uliopita, alikataa kujiongeza muhula mpya katika uchaguzi wa urais na kukubali kukabidhi madaraka kwa waziri wake wa zamani wa ulinzi, Joao Lourenço.

Hata hivyo, aliendelea kushikilia uongozi wa chama tawala cha MPLA, nafasi ya kuchukua urais kwa utaratibu wa mamlaka ya uongozi wa nchi.

Siku ya Jumamosi kipenzi huyo nambari moja wa Angola, mwenye umri wa miaka 76 atakabdhi funguo za chama kwa Rais Joao Lourenço katika mkutano wa chama.

“Kustaafu kwa dos Santos ni hatua muhimu katika mabadiliko ya kisiasa nchini Angola,” amesema mchambuzi Alex Vines kutoka kituo cha tathimini cha Uingereza cha Chatham House.

Ndugu zake wamekua wakidhibiti sekta muhimu za uchumi, kama vile kampuni ya mafuta ya kitaifa iliyomilikiwa na binti yake bilionea Isabel, na washirika wake wa karibu walikuwa wakisimamia jeshi na polisi.

Lakini, kwa mshangao mkubwa, mtu ambaye alikuwa kama mtu wake wa karibu, Joao Lourenço haraka alijitoa aliamua kuondokana na mamlaka ya mtangulizi wake kwa kushambulia kwanza mizizi ya utawala wa dos Santos.

Kwa kukabiliana na mdororo wa uchumi na kupambana na rushwa, rais wa sasa aliamua kumtenga Isabel dos Santos (binti yake Jose Eduardo Dos Santos), kwenye usimamizi wa kampuni ya Sonangol na kaka yake Jose Filomeno, anayejulikana kama ‘Zenu’, kwenye mfuko wa kitaifa la nchi.

Katika miezi michache,ndugu na jamaa wengi kutoka ukoo wa dos Santos wameondolewa kwa makini kutoka kuwa wakuu wa taasisi, makampuni ya umma na chama, ambapo Jose Filomeno naye pia alishtakiwa kwa kosa la ubadhirifu mali ya umma.

Hali hii ilizua mvutano mkubwa mpaka Rais huyo wa zamani mwenyewe alionyesha hasira yake hadharani.

“Mabadiliko ni muhimu lakini hayapaswi kuwa kuwa yenye msimamo mkali,” alisema dos Santos mnamo mwezi Desemba mwaka uliopita.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.