DKT.BASHIRU “MKUU WA MKOA ATAKAYESHINDWA KUSIMAMIA HAKI ZA BODABODA NA MACHINGA HANA KAZI”

Na Allawi Kaboyo-Bukoba.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi  CCM Daktari Bashiru Ally Kakurwa, amewataka watendaji wa Serikali hususani wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini,  kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa haki wakati wa kuwatumikia Wananchi wao pasipo kulegalega.

Kauli hiyo ameitoa desemba 22 mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchama wa chama hicho waliojitokeza kumlaki alipowasili mkoani Kagera

na kumtolea mfano Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kwa Nidhamu, Uzalendo, Ujasiri na Uchapakazi wake uliotukuka aliouonyesha kwa Kipindi Kifupi toka Ameteuliwa.

“Niwaombe wananchi wa mkoa wa Kagera tumpe ushirikiano mkubwa mkuu wetu wa mkoa mpya, ni kijana mwenye nidhamu,mzalendo na mchapakazi, na nitumie mfano wake kutuma salamu kwa wakuu wa mikoa wote nchi kumuiga mkuu huyu wa mkoa kwa kuchapa kazi kwa haki na uzalendo wakati wa kuwahudumia wanancnhi” alisema Dkt.Bashiru

Dkt. Bashiru amezidi kuwakumbusha Watendaji hao wakiwemo Jeshi la Polisi kutowabugudhi wajasiliamali wadogo  na Boadaboda, na kuwaomba wajasiliamali hao kuunga Mkono Kampeni iliyoanzishwa na Mh. Rais John Pombe Magufuli ya vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, sambamba na Kampeni ya Kulipa KODI.

Kwa upande Mwingine Dkt. Bashiru, Ameshangazwa na Baadhi ya Mazao ya Biashara yaliyokufa likiwemo zao la Chai, ambalo amelitaja kuwa chachu ya Mafanikio yake ya kimaisha, na kueleza kuwa anatamani kuona watoto wengine wa Wakulima nao wakifanikiwa kupitia zao hili pamoja na Kahawa, hivyo ametaka kupata majibu ya nini kilichotokea juu ya zao hilo kabla ya Kuondoka Mkoani hapa.

“Mimi nimesoma hadi kuyafikia mafanikio niliyonayo sasa kwa kulitegemea zao hili la chai,natamani kuona watoto wa wakulima wa zao hili pamoja na kahawa na wao wakinufaika kama nilivyonufaika mimi, kwa mantiki hiyo nataka kabla ya kuondoka hapa nipate majibu yanayoridhisha ni kwanii zao hili limekufa.” Alieleza Dkt.Bashiru.

Akitoa salaamu zake kwa wananchi waliojitokeza wumpokea, wyumbani kwake Kanazi – Kemondo, Dkt.Bashiru amesema kuwa anatarajia kukutana na halmashauri kuu za wilaya zote kwa kufanya nao Vikao, pamoja na halmashauri kuu ya mkoa ambapo pia ameela kuwa atakutana na viongozi wa halmshauri ya eilaya ya Bukoba, katika kikao mahsusi kujadili kile alichokiita mgogoro wa kipuuzi juu ya mvutano wa wapi panastahili kujengwa hospitali ya wilaya ya Bukoba.

Aidha Dkt.Bashiru amewataka viongozi wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba kumaliza tofauti zao mapema kabla  hajakutana nao, kwani hatua kali zaweza kufuata kulingana na taratibu za Chama zilivyo,na ikiwa watashindwa kukubaliana, Pesa Iliyopangwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo kiasi cha shilingi Bilioni 1 itapelekwa sehemu nyingine.

Dkt. Bashiru Ally amewasili Mkoani Kagera Desemba 22 kwa Mapumziko mafupi,  huku akipanga pia kukutana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani hapa,  katika kujadili Mustakabari wa Chama na Shughuli za Kichama Mkoani Kagera.

Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi mkoani Kagera wakiwa wamsubiri Dkt.Bashiru Ally katika kiwanja cha ndege Bukoba.
Dkt.Bashiru Ally kushoto akisalimiana na mwenyekiti wa CCM wilaya Bukoba mjini mhe.Joas Mganyizi Zachwa kulia Mara baada ya kuwasili katika kiwanja cha ndege Bukoba.

 

 

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.