DKT.ABBASI AMUUNGANISHA DKT. MWINUKA WA TANESCO ‘LIVE’ REDIONI KUFAFANUA MIKAKATI YA TANESCO

Dodoma.

Wakati serikali ya awamu ya tano ikifanya mageuzi kuelekea Tanzania ya viwanda,mkurugenzi mtendaji wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, amesema kuwa shirika hilo limepanga kuzalisha megawati zaidivya 5,000 ili kuwa chachu ya Tanzania ya viwanda.

Dkt. Mwinuka ameeleza mikakati hiyo jioni hii baada ya kupigiwa simu na .semaji mkuu wa serikali, Dkt. Hassan Abbasi, aliyekuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi maalum cha moja kwa moja (Live) na redio RASI FM ya jijini Dodoma, ambapo mtendaji huyo wa Tanesco akijibu hoja zilizoibuliwa alisema katika miaka mitatu Tanesco imetekeleza miradi ya kuzalisha na kusafirisha umeme nchini.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni Kinyerezi I extension, Kinyerezi II na sasa maandalizi ya kuzalisha megawati 2,100 katika mradi wa Stiglers Gorge yameanza.

Dkt. Mwinuka akizungumzia ofisi yake na yeye mwenyewe kuhamia Dodoma wiki hii anasema sasa wana fursa ya kutoa huduma bora zaidi kwa makao makuu ya nchi ambapo hivi sasa tayari wamefikisha umeme kwenye eneo la Ihumwa zilikoanza kujengwa nyumba na ofisi za serikali.

“Dodoma ni jiji linalozidi kukua, watu wanaongezeka na majengo mengi ya serikali yatajengwa, hivyo tunahitaji kuongeza nguvu ili watu wote wafikiwe na umeme,” ameeleza Dkt. Mwinuka.

Kwa upande wake msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, amezihimiza Bodi za Mazao nchini kuhakikisha zinamsaidia mkulima kuzalisha bidhaa zenye ubora pamoja na kumtafutia masoko ya uhakika kama walivyoagizwa na Rais Magufuli kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

Dkt. Abbasi amesema kuwa serikali imeendelea kumsaidia mkulima kwa kuanzisha soko la bidhaa, taasisi ambayo inaratibu minada ya mazao ya wakulima ili kumpata mnunuzi ambaye atatoa bei nzuri kwa wakulima.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.