DIWANI MNEMELE:MICHEZO ITUMIKE KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA.

Na Stephen Noel,Mpwapwa.

Jamii imeombwa kutumia njia za michezo katika kutoa mafunzo rika kwa vijana ili kuweza kuwafikia vijana wengi.

Rai Hiyo imetolewa hii Leo na Pamela Mnemele diwani wa viti maluum tarafa ya Kubakwe wakati akifungua bonanza la michezo lililoandaliwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la TAYOA (Tanzania Youth Alliance) Jimbon Kibakwe.

Bi Mnemele alisema kwa kutumia michezo kunaweza kuwavuta mabinti wengi kupata Elimu iliyo andaliwa kutokana na vijana wengi kuvutiwa na mchezo hivyo hurahisisha ujumbe kufika kwa kundi kubwa na kwa urahisi zaid tofauti na njia za mikutano ambayo vijana wengi hasa mabint wanakuwa hawaudhurii mikutano hiyo.

Aidha Bi Mnemele amesema kuwa nonanza hilo lenye lengo la kuwajengea uwezo mabinti Katika kuweza kupambana na elimu ya ugonjwa wa UKIMWI,ukatili wa kijinsia,zambamba na zoezi la upimaji Virus vya Ukimwi na zaratani ya mlango wa kizazi.

Kwa upande wake mratibu wa TAYOA mkoa wa Dodoma bwana Frank Kilumba amesema bonanza hilo limejenga kuutambulisha mradi wa uhamasishaji wa mabinti ambao ni kundi barehe la mabinti walio ndani na nje ya shule kuweza kuvikabili vikwazo vya ubinti ili  kufikia malengo yao ya kimaisha.

Hata hivyo Bwana Frank amesema endapo jamii na mabinti hao wakaupokea mradi huo kwa mtazamo chanya utaweza kupunguza mimba mashuleni na ndoa Katika umri mdogo.

“Unajua tumeamua kutumia michezo kutokana na mchezo inamjengea binti kujiamini lakin pia kukabiliana na changamoto zinazo wakabili “aliongea Frank

Pia Bonanza hilo liliambatana na utoaji wa vifaa vya michezo kwa shule ya msingi Kibakwe na shule sekondari Kibakwe.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.