DC NEWALA AKAMATA KOROSHO KUTOKA MSUMBIJI.

 

Siku moja tu baada ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli kutangaza kuwa Serikali itanunua korosho kwa bei Tshs 3300/= kwa kilo moja na zoezi kusimamia Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ) huku akipiga marufuku uingizwaji wa korosho kimagendo kutoka nje ya Tanzania.

Mkuu wa Wilaya Mhe. Aziza Mangosongo amemkamata mtu mmoja leo akiingiza korosho kimagendo magunia zaidi 90 yenye kilo zaidi 100 kila moja katika maeneo ya Mpakani akivusha korosho wakati wa Operation maalumu inayoendelea Wilayani humo.

Mhe. Aziza aliongozana na wajumbe
wa kamati ya ulinzi na Usalama ya wilaya pamoja na wakurugenzi wa halmashauri zote za Newala katika Operesheni hiyo.

“Naomba wananchi muendelee kutoa ushirikiano kwa Serikali kuendelea kufichua vitendo vichafu kutaka kuihujumu nchi na ukiukwaji wa Sheria” amesema Mhe. Aziza.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.