DC MWAIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA KATA, VIJIJI NA VITONGOJI.

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Bw. Rashid Mohamed Mwaimu amefanya kikao cha pamoja na viongozi wa kata zote, vijiji pamoja na vitongoji ndani ya wilaya yake.

Mheshimiwa Mwaimu amekutana na viongozi hao mapema siku ya jana Septemba 5, 2018, ambapo alitumia fursa hiyo kusikiliza kero mbalimbali pamoja na changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa miradi mbalimbali wilayani humo.

Kikao hicho kimefanyika baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika kata hizo ili kujiridhisha na hatua zinazochukuliwa katika utekelezaji wa miradi hiyo sambamba na thamani ya pesa (value of money) zinazotumika katika miradi hiyo.

[Picha kwa hisani ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya]
[Picha kwa hisani ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya]

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.