DC LUOGA AANZISHA MICHEZO ILI KUTETEA UHURU WA MTOTO WA KIKE

Na Frankius Cleophace Tarime

Mkuu wa wilaya ya Tarime  Glorious Luoga ameanzisha bonanza la Michezo mbalimbali huku kauli mbiu ikiwa ni kutetea na kulinda haki za mtoto wa kike ambapo timu 12 za mpira wa miguu kwa wanaume zinashiriki pia na timu Nne za Wanawake zinashiriki mpira wa miguu katika viwanja vya Chuo cha Ualimu TTC Mjini Tarime.

Luoaga amesema kuwa katika wilaya ya Tarime mwanamke amekuwa hakinyimwa uhuru pamoja na mtoto wa kike hivyo kupitia michezo hiyo mashirika na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia watatumia michezo hiyo ili kutaoa elimu juu ya madhara ya ukatili ili kulinda na kutetea mtoto wa kike wilayani Tarime Mkoani Mara.

“Michezo hii kilele chake ni tarehe tisa Desemaba mwaka huu siku ya Uhuru hivyo nimetumia siku hiyo ya uhuru ili kulinda na kutetea uhuru wa mtoto wa kike hapa Tarime badomtoto wa kike hajapata uhuru pia michezo yote itakuwepo kama vile kukimbia, kilometa ndefu na fupi, Mpira wa pete, kukimbia kwenye magunia na kukimbiza kuku katika viwanja vya chuo cha ualimu alisema Luoga”.

Vile vile Mkuu wa Wilaya ya Tarime ameongeza kuwa Michezo hiyo itaboresha mahusiano baina ya Jamii na watumishi wa serikali katika wilaya ya Tarime kwani nao wanashiriki Michezo hiyo.

Jovitus Alphonce ni afisa miradi kutoka shirika la Jukwaa la utu wa Mtoto CDF Tarime amesema kuwa wao kama shirika wanaendelea kushirikiana na serikali kulinda na kutetea haki za mtoto wa kike hivyo kupitia Tamasha hilo la michezo wao kama wadau wataendelea kupinga ukatili.

Alphonce ameongeza kuwa wanatumia siku 16 za kupinga ukatili kutoa elimu pia kupitia michezo hiyo kwa kuwa pia mwaka huu ni wa ukeketaji hivyo lazima watumie mbinu zote ili kuokoa mtoto wa kike.

Kwa upande wake Shaban Shaban kutoka Shirika la Plan Intertaniona akieleza jinsi amabvyo wanatumia michezo kufikisha ujumbe amedai kuwa michezo imekuwa ikikusanya watu wengi hivyo kupitia mikusanyiko hiyo wanatoa elimu ya kupinga ukatili wa aina zote ikiwemo ukeketaji kwa mtoto wa kike na kuhakikisha wanamlinda mtoto huyo ili aweze kupelekwa shule ili kutimiza ndoto zake za kimasomo.

Katika uzinduzi wa Mashindano hayo Tarime Veteran imeminyana vikali na Timu ya Halmashauri ya Mji wa Tarime ambapo Timu ya Halamshauri ya Mji wa Tarime imeibuka kidedea kwa kuilaza timu ya veterans kichapo cha bao 4-2.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.