DC KINONDONI AHAMISHIA OFISI KWA WANANCHI

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh Ally Hapi ameambatana na wakuu wa idara mbalimbali kutoka ofisini kwake na kuanza nao ziara ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa wilaya hiyo.

Katika ziara hiyo iliyoanza leo katika kata ya Tandale ambapo mkuu huyo wa wilaya ameweza kusikiliza kero za wananchi waishio maeneo hayo,katika utangulizi wake alisema ni jukumu lake kuwasikiliza na kuzitatua kwani ndiyo jukumu ambalo rais kamuagiza kulifanya.

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mh Ally Hapi akiwa katika ziara yake kata ya Tandale.

‘’Nimejipanga na timu yangu kuanza ziara yangu na nitazunguka kata hadi kata kuwatembelea wananchi na kusikiliza kero zinazowakabili wananchi wangu, hiyo ndo kazi nimepewa kama mkuu wenu wa wilaya.

Serikali ya awamu ya tano inafanya mambo mengi sana na kwa sababu serikali ni kubwa inawezekana sisi tukikaa juu tusijue yanayoendelea huku chini vizuri, wapo wananchi wanaoteseka kwa kukosa haki zao, wananchi ambao wananyanyasika, wananchi wenye kero mbalimbali zinazohusu maji, afya, elimu, ardhi, jeshi la polisi na n.k. Kwasababu mimi sio mtu wa kukaa ofisini nimeamua kuanzaisha huu mchamchaka kata hadi kata kuwasikiliza wananchi’’ – Ally Hapi

Katika ziara hiyo wananchi waliibua kero zao mbalimbali zikiwemo huduma mbovu katika Zahanati ya Tandale, ukosekanaji wadawa katika Zahanati hiyo, migogoro ya ardhi, tatizo la maji, wazee kutopata fedha zao stahiki na kupewa watu wanaojiweza, migogoro ya mirathi, shutuma za polisi jamii kuwapiga wananchi kinyume na sheria, ujenzi wa barabara, ujenzi wa shule ya sekondari katika kata hiyo na kadhalika.

Aidha DC Ally Hapi ametoa maagizo kwa wakuu wa idara husika kushughulikia kero hizo za wananchi za kuhakikisha zimepatiwa ufumbuzi wa kina ili wananchi wa kata hiyo wasiendelee kuteseka na kujivunia nchi yao.

Katika hali nyingine wananchi wa maeneo hayo walionekana kufurahishwa na ziara ya mkuu huyo wa wilaya kwani walikua wanatamani sana kukutana nae ili waeleze kero zao mbele yake lakini ikawa inawapa ugumu hivyo wamemshukuru.

Mkuu huyo wa wilaya atafanya ziara ya kuzunguka na kusikiliza kero za wananchi kwenye kata zote 20 katika wilaya ya Kinondoni.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.