DC.KATAMBI AAHIDI KUENDELEZA MAPAMBANO KWA WAVUNJAJI SHERIA DODOMA


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi, amesema yuko tayari usiku na mchana kupambana na kila aina ya uhalifu na ukiukwaji wa sheria Jijini Dodoma.

“ Kwa Dodoma Wahalifu,  wazembe, wabadhirifu, wapiga deal, wala rushwa, wakwepa kodi, wachafuzi na waharibifu wa mazingira pamoja na wavunja haki za binadamu hasa kwa wanyonge hawana nafasi hapa na hatutawavumilia hata sekunde moja.

“ Vyombo vyetu vipo imara kulinda mda wote haki za Raia, za Serikali, Taasisi na makundi yote,” amesema DC Katambi.

Amesema ni muda wa kuchapa kazi na kujenga nchi kama Rais Dk John Magufuli anavyoonesha mfano wa uzalendo kwa kujenga Nchi na sio kujenga watu binafsi au vikundi, wakoloni na vibaraka wao.

“ Vijana tuko tayari kulitumikia Taifa Tanzania. Nchi kwanza na hapa kazi tu,” amesema DC Katambi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.