CROATIA WAIFATA UFARANSA FAINALI KOME LA DUNIA

Nchini Urusi ,mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya timu ya taifa ya Uingereza dhidi ya timu ya taifa ya Croatia umekwisha kwa timu ya taifa ya Croatia kujihakishia ticket ya kucheza fainali ,tarehe 15/07/2018 katka dimba la Luzhnik ndani ya jiji la Moscow.

Katika mchezo huo timu ya taifa ya Uingereza ilikuwa ya kwanza kujiandikiwa goli katika kipindi cha kwanza kupitia kwa mlinzi wa klabu ya Tottenham K. Trippier kwa adhabu ndogo  iliyomshinda  mlinda mlango  wa Croatia Danijel Subasic nakukwama nyavuni, kipndi cha pili Croatia walirejea mchezoni baada ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya  Inter Milan , Ivan Perisic kukomboa   goli dakika ya 68.

Mpaka dakika ya tisini mchezo ulikwisha kwa sare pacha ya 1-1, kabla ya mwamuzi ajaongeza dakika 30 .

Dakika ya 109 mshambuliaji wa klabu ya Juventus ya nchini Italia Mario Mandzukic aliandikiwa Croatia goli la pili, goli ambalo liliwapa ticket ya kucheza fainali.

Sasa Croatia inakuwa nchi ya pili yenye idadi ndogo ya watu kucheza fainali ya kombe la dunia.

Raisi wa nchi ya Croatia bi  Kolinda Grabar-Kitarović akuwepo uwanjani kama ilivyo desturi yake alikuwa kwenye majukumu mengine ya taifa lakini amehaidi kuwepo kwenye mchezo wa fainali siku ya jumapili  katika dimba la Luzhniki kuipa timu yake hamasa katika mchezo huo.

 

 

 

khalidchukuchuku

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.