CHUPA ZA DAMU 601 ZINAHITAJIKA MKOANI NJOMBE ILI KUKIDHI MAHITAJI

Na Amiri kilagalila

Zaidi ya chupa za damu 550 zinahitajika mkoani Njombe ili kukidhi mahitaji yote kwa mwezi ambapo jumla ya chupa 470 tu kati 601 ndio zinazo kusanywa huku kukiwa na upungufu wa chupa 131 hali inayowalazimu waratibu wa damu salama kuiomba jamii kujitokeza katika zoezi la uchangiaji ili kuwasaidia wenye mahitaji hayo.

Akizungumza na mtandao huu wakati jeshi la polisi pamoja na waandishi wa habari wakichangia damu,Mratibu wa Damu Salama Mkoa wa Njombe Bi.Prisca Ndiasi amesema Wanalazimika Kuendesha Zoezi hilo Muhimu Kutokana na Upungufu Mkubwa wa Damu.

“Mpaka sasa tunauwezo wa kukusanya chupa 470 hadi 480 kwa mwezi kwa hiyo bado tunauhitaji tunaiasa jamii na wananchi wa Njombe kujitokeza na kuchangia damu kwa hiari kwa kuwa bado tuna uhitaji mkubwa”alisema Prisca Ndiasi

Kwa kuona umuhimu huo Ili Kukabiliana na Tatizo la Upungufu wa Damu Kwa Wagonjwa Mkoani Njombe Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limeungana na Wakristu wa Dhehebu la waadventista wasabato Kuchangia Damu Baada ya Wakristo Hao Kutekeleza Zoezi Hilo Disemba 26 Mwaka Huu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Renatha mzinga Katika Bwalo la Jeshi hilo Wamechangia Damu Ili Kuunga Mkono Jitihada Hizo Kwa ajili ya Kusaidia Wagonjwa wenye mahitaji ya Damu.

“Pamoja na misaada mingine na huduma ya ulinzi ambayo tumekuwa tukiitoa kwa wananchi wetu lakini na sisi leo tumeona umuhimu wa kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia ndugu zetu wanaopata matatizo, niwaombe askari wajitokeze kwa wingi ili tuendelee kuisaidia pia hospitali yetu ya kibena”alisema kamnda mzinga.

Baadhi ya Askari Walioshiriki Kuchangia Damu Wanasema Wamewiwa Kuwasaidia Wagonjwa Baada ya Kuhamasishwa na Wataalamu wa Afya Toka Hospitali ya Rufaa Ya Mkoa wa Njombe Kibena.

“Nimechangia damu kutokana na uhamasishaji unaondelea kwasababu kuchangia damu maana yake umeisadia jamii yote kwa ujumla, watu wakipata ajali wanapoteza damu nyingi kwa hiyo tunavyo zidi kuchangia naamini itaokoa maisha yao.”alisema mmoja wa Askari

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.