CHELSEA WAIFANYIA MANCHESTER CITY KITU MBAYA

 Baada ya kuzagaa kwa taarifa za kiungo wa klabu ya Napoli Jorginho kujiunga na klabu mabingwa wa ligi kuu nchini Uingereza ,Manchester city . Jana katika mji wa Capri nchini Italia kulikuwa na kikao  kati ya raisi wa klabu ya Napoli Aurelio De Laurentiis  na mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abrahamovic  wawili hao wamefikina makubalinao ya Chelsea kupata saini  ya Kiungo wa Napoli Jorginho na aliyekuwa mkufunzi wa Klabu hiyo Maurzio Sarri kwa dau la paundi million 65, paundi million 8 kwa kocha Sarri na 57 kwajiri ya kiungo Jorginho.

Kujiunga kwa Sari ndani ya klabu ya Chelsea maana yake aliyekuwa mkufunzi wa klabu hiyo muitaliano mwenzake Antonio Conte ataondoka kunako klabu hiyoo muda wowote kutoka sasa.

Pia uongozi wa klabu ya Chelsea umewatoa shaka mashabiki klabu hiyo wanaodhani kwamba Chelsea itawachia viungo wake washambuliaji Eden Hazard na Willian. Hazard ananyemelewa na klabu mabingwa Ulaya Real Madrid ambayo inamwona Hazard kama ni mbadala wa mshambuliaji Christian Ronaldo anayekariabia kujiunga kunako klabu ya Juventus.

Willian yeye ananyemelewa na klabu ya Manchester united kujiunga nao .

Jorginho na Sarri walikuwa na msimu mzuri , kwenye msimu ulioisha wa ligi kuu nchini Italia maarufu kama Seria A, kwani waliisaidia klabu ya Napoli kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Italia wakiwa na alama 90 alama 5 nyuma ya mabingwa wa ligi hiyo Juventus walijikusanyia alama 95.

 

 

khalidchukuchuku .

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.