CHAMA KIKUU CHA UPINZANI AFRIKA KUSINI ‘DA’ KUPINGA MAREKEBISHO YA KATIBA MAHAKAMANI.

 

Pretoria, AFRIKA KUSINI.

Chama kikuu cha upinzani nchini Afrika Kusini cha Democratic Alliance (DA), kimetangaza kuwa kitaenda mahakamani kusimamisha pendekezo la kufanyika marekebisho ya ardhi baada ya Bunge kupasisha ripoti inayoidhinisha kufanyika marekebisho ya katiba yatakayoruhusu kutwaliwa ardhi zinazomilikiwa na wazungu waliowachache bila ya kulipwa fidia.

Chama cha Democratic Alliance (DA) na baadhi ya makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali mpango huo wa serikali ya Pretoria yakisisitiza kuwa, utahatarisha haki ya kumiliki na kuwatia woga wawekezaji wa kigeni.

Umiliki wa ardhi na mashamba ni suala nyeti sana nchini Afrika Kusini ambako ubaguzi wa rangi ungali umekita mizizi baada ya miongo miwili ya kuondolewa madarakani utawala wa ugauzi (Apartheid), uliowapokonya wazalendo weusi mashamba yao na kuyagawa kwa wazungu waliowachache.

Kwa msingi huo mwezi uliopita timu ya Bunge la Afrika Kusini ilitoa pendekezo la kufanyika marekebisho ya katiba yatakayowezesha kutwaliwa ardhi kubwa na mashamba yanayomilikiwa na wazungu wachache bila ya kulipwa fidia.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini aliyechukua nafasi ya Jacob Zuma mwezi Februari mwaka huu, amelipa kipaumbele kikubwa suala la kugawa ardhi kwa wazalendo weusi katika jitihada zake za kukiunganisha tena chama tawala cha ANC na kupata uungaji mkono wa umma kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika hapo mwakani.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.