CHADEMA YAPATA PIGO LINGINE LONGIDO

Chama Cha CHADEMA katika wilaya ya Longido Leo Jumatatu Januari 08/01/2018 kimepata pigo lingine baada ya diwani wa kata ya Olmolog, Dio Lomayan Laizer kujiuzulu wadhifa wake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Pamoja na diwani huyo, wafuasi wengine zaidi ya 130 wa chama hicho wakiwemo viongozi wa CHADEMA kata wamejiunga na CCM kwenye mikutano mbalimbali ya hadhara ya kampeni za mgombea ubunge kupitia CCM katika tarafa ya Ketumbeine.

Kwa muda mrefu sasa tangu Rais Magufuli aingie madarakani chama cha CHADEMA kimepoteza wanachama wengi ambao wamekuwa wakijiunga na CCM ili kuunga mkono jitihada za kukomesha ufisadi zinazofanywa na Rais huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama hicho taifa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.