CHADEMA YAIONDOA MAHAKAMANI KESI YA UCHAGUZI

Dar es salaam.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kimeiondoa mahakamani kesi ya uchaguzi namba 5/2018 iliyofunguliwa Mahakama kuu kanda ya Tanga ya kupinga uchaguzi wa marudio jimbo la Korogwe vijijini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano CHADEMA,Tumaini Makene,imesema wameiondoa kesi hiyo baada ya kufanya uchambuzi wa kina ukihususha ushauri wa kitaalam kutoka kwa mwanasheria wa chama hicho.

Katika kesi hiyo iliyokuwa ianze kutajwa Desemba 10, mwaka huu, aliyekuwa mgombea wa CHADEMA,ndugu Aminata Saguti alikuwa akilalamikia mchakato ulivyoendeshwa kwa kukiuka taratibu za uchaguzi na mamlaka husika, kuanzia hatua ya uteuzi wa wagombea hadi kutangazwa kwa matokeo.

Ndugu Saguti pia alikuwa amelalamikia namna mchakato huo ulioendeshwa kinyume cha sheria, ulivyo muhujumu na kumnyima haki yake ya kuteuliwa kugombea nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo uliofanyika Septemba 16, mwaka huu.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa,baada ya mashauriano, chama kimeielekeza kurugenzi ya sheria, kulifanyia kazi suala hilo kwa namna nyingine mbadala, kupitia mahakamani, ambayo imeonekana kuwa itafaa katika kuhakikisha haki ya wananchi wa Korogwe vijijini iliyoporwa wazi wazi mchana kweupe, inapiganiwa kwa nguvu zote ili hatimaye ipatikane kupitia mkondo wa kisheria.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.