CCM YAJIHAKIKISHIA USHINDI VINGUNGUTI, NGOME YA UPINZANI YAANGUKA

Dar es Salaam

Wenyeviti saba wa Serikali za mtaa kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) na Chama cha Wananchi (CUF) kata ya Vingunguti wamejivua nyadhifa zao na kujiunga na chama cha Mapinduzi (CCM ) kwa lengo la kumuunga mkono mgombea udiwani wa kata hiyo, Omary Kumbilamoto.

Wenyeviti hao, wametoa uamuzi huo katika mkutano wa kampeni wa kugombea udiwani, uliofanyika Relini ambapo wakizungumza baada ya kukabidhi kadi zao kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM ) mkoa, Kate Kamba wamesema wameamua kufanya hivyo baada ya kuchoshwa na migogoro iliopo ndani ya chama cha CUF,

Kwa upande wake, Mbunge wa jimbo la Segerea Bonah Kalua amesema kuwa, alikua hawezi kushirikiana na aliyekuwa Diwani kutokana na kila mmoja alikua na ilani ya chama chake lakini kwa sasa anaahidi kuwa nae bega kwa bega

“Nawaomba wananchi mumpigie kura Kumbilamoto kwani alichokifanya kitendo sahihi cha kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt , John Magufuli kutokana kukuona kwa macho na vitendo anayoyafanya.”amesema Bonah.

Kwa upande wake, Mgombea udiwani wa kata hiyo, Omary Kumbilamoto, wakati akiomba kura amesema atahakikisha walemavu wote wanapata mkopo unaotolewa na halmashauri ili kuweza kujiendeleza katika biashara zao na kuondokana na hali ya utegemezi.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.