CCM NYAMAGANA YAMUENZI BABA WA TAIFA KWA UPANDAJI WA MITI

MWANZA.

Na Mwandishi wetu

Taifa la Tanzania tunapo elekea Kilele cha siku ya Nyerere kuadhimisha miaka 19 toka Baba wa taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere atangulie mbele za haki,  Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana kikiongozwa na Katibu Wilaya Ndg. Salum Kalli pamoja na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula hivi leo wamenzi siku hii kwa upandaji wa miti 1000 shule mbili za Msingi Mkolani pamoja na Ibanda kwa uratibu wa Umoja wa Vijana tawi la Chuo Kikuu Huria Tanzania.

Akifungua maadhimisho hayo Katibu Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndg. Salium Kalli alisema historia ya taifa la Tanzania limejisimika katika Misingi imara ya mwaasis wa taifa hili Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliyehamaisha upandaji wa miti katika uongozi wake wa awamu ya kwanza kwa dhima ya Miti ni Uhai.  “Nina wapongeza tawi la Chuo Kikuu Huria Tanzania Umoja wa Vijana wa CCM kwa kumuenzi Baba wa taifa kwa Vitendo kwa upandaji wa Miti”  Kalli amesema.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Nyamagana  Mhe Stanislaus Mabula ametumia hadhara hiyo kuwaasa wanafunzi na uongozi wa shule hizo mbili kutunza miti hiyo ili kuwa kielelezo cha uwepo unaoishi vizazi na vizazi. Kadharika aliwaasa wana Nyamagana kupenda tabia za upanda miti ya matunda na kivuli kusaidia uoto wa asili pamoja na mazingira safi.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi tawi la Chuo Kikuu Huria Ndg. Kuruthumu amesema wamewiwa kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa kushirikiana na wanafunzi wa shule mbili za msingi kwa dhamira yakuwakumbusha vijana hao wapi taifa hili limetoka.

Kwa nyakati tofauti tofauti Mwl Mkuu Shule ya Msingi Mkolani Mwl Neldomina Nyirenda pamoja  na mwalimu mkuu wa shule Ibanda Mwl Bhati Parapara Ibanda wameshukuru Chama Cha Mapinduzi kupitia umoja wa Vijana tawi la Chuo Kikuu Huria kumenzi Baba wa Taifa kwa upandaji wa Miti.

Aidha Wameomba wasichoke kuendelea kuwashirikisha shule hizo zipo tayari kushirikiana na taasis zozote kwa mstakabali wa ustawi wa elimu bora.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi ngazi wilaya, Kata na matawi, uongozi wa shule ya Msingi Mkolani na Isibanda pamoja na mtendaji wa Kata na Mitaa.

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana wakishiriki zoezi la upandaji miti.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.