CCM MKOA WA MWANZA YAENDESHA SEMINA YA USAJILI KUPITIA MFUMO WA DIJITI

Mwanza

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza, leo kimeendesha semina ya kutoa mafunzo maalum kwa washiriki wa zoezi la uandikishaji wanachama wa chama hicho na Jumuiya zake tatu katika mfumo dijitali mtandao.

Semina hii ya siku tatu imewakutanisha washiriki kutokea wilaya sita zikiwemo Nyamagana, Ukerewe, Magu, Misungwi, Kwimba pamoja na Sengerema.

Akizungumza katika semina hiyo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Salum Kalli amesema uandikaji uanachama kupitia mfumo mpya wa digitali ulianzia wilayani Ilemela ambao utawezesha mkoa wa Mwanza kuwa miongoni mwa mikoa minane nchini kuanza kutoa huduma hii.

Aidha amesema kuwa, kwa wanachama wote pamoja na jumuiya zote za Umoja wa wanawake, Vijana na wazazi na kumwezesha mwanachama kuwa na kadi moja ya unachama yenye taarifa zake zote kwa kutumia mfumo wa kidijitali.

Semina hii imefanyika wilayani Nyamagana chini ya mkufunzi Joseph Mtinangi kutokea makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi, ambapo wilaya zote zimekabidhiwa vifaa maalum kwaajili ya uendeshaji zoezi hilo kiufanisi na kiuweledi.

Hata hivyo, viongozi mbalimbali wamehudhuria ikiwemo makatibu wa chama hicho kutokea wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, ikiwa ni wilaya za Kwimba, Misungwi, Ukerewe, Magu, Sengerema na Nyamagana.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.