CHADEMA KANDA YA NYASA KUKUTANA NA WANAHABARI KUZUNGUMZIA UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI ,IRINGA NA TUNDUMA

WAKATI kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata tatu kati ya tano za Manispaa ya Iringa zikitaraji kuanza huku Tunduma chadema wakilalamika mchakato wa uchukuaji na urejeshaji fomu chadema kanda ya Nyasa kuzungumza na wanahabari. Katika taarifa iliyotolewa na chama hicho jioni ya Leo inasema mwenyekiti wa kanda ya Nyasa Mchungaji Peter Msigwa ataongozana na katike kanda kueleza mengi kinachoendelea. Mkutano huo umepangwa kufanyika mjini Iringa na undani wa nini kimejiri usikose kutembelea mtandao huu wa DarmpyaBlog.

Soma Zaidi >>

HALMASHAURI YA IRINGA YAJIPANGA KUTEKELEZA KERO ZA MAJI KWA WANANCHI

    wananchi  wa  Migori  Ismani wakipata  huduma ya  maji katika  pampu iliyowekwa  kijijini hapo ,japo kwa  sasa mradi mkubwa wa maji ya bomba  unatekelezwa . HALMASHAURI  ya  Manispaa ya  Iringa  mkoani Iringa  imejipanga  kuendelea  kutekeleza  ilani ya  uchaguzi ya  chama  cha mapinduzi  (CCM) ya  utekelezaji wa  miradi ya  maji kwa  wananchi . Mkurugenzi wa  Halmashauri  ya  Iringa  Robart Masunya  aliueleza  mtandao  huu wa Dar Mpya  kuwa  tayari  wameendelea  kutekeleza  miradi ya maji katika maeneo mbali mbali na  kuwa lengo ni  kufikia asilimia  100 ya  utekelezaji  wa ilani  ya  CCM.…

Soma Zaidi >>

ALIYEWATAPELI WATALII DOLA 5000 AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia Omwailimu Sosthenes ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Utalii ya  Arise Special Sunrise,kwa tuhuma za kuwatapeli watalii wawili Dola za kimalekani 5000. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, DCP Liberatus Sabas, amesema mtuhumiwa huyo aliwatapeli watalii hao ambaye mmoja anaishi Marekani na mwingine nchini India kwa makubaliano kwamba angewapeleka safari ambazo walizipanga. Amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuwatapeli wageni hao aliwatelekeza katika nyumba ya wageni maeneo ya Sinza na walipojaribu…

Soma Zaidi >>

MAUZO DSE YAPOROMOKA

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kutoka Sh bilioni 1.11 wiki iliyopita hadi Sh milioni 676.26 wiki hii. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Emanuel Nyalali, amesema mauzo hayo yametokana na kuuzwa kwa mihamala 166. “Wakati huo thamani ya Soko la Hisa imeongezeka hadi kufikia Sh trilioni 22.18 kutoka Sh 21.99 wiki iliyopita,” amesema Nyalali. Aidha amesema katika kipindi hicho, hatifungani za serikali na makampuni zenye thamani ya Sh bilioni 1.96 ziliuzwa kwenye mihamala…

Soma Zaidi >>

KIKUNDI CHA GROUP LA WHATSAPP KINACHOTOA HUDUMA ZA KIJAMII

Imezoeleka kwamba magroup mengi ya mitandao hasa mtandao wa Whatsap ni kwa ajili ya kuchati kwa kubadilishana mawazo, kupashana habari, kukutanisha marafiki wapya na mengine mengi, ila hii imekuwa ni tofauti kabisa na kundi (group) hili. Group la Whatsap hilo linalojulikana kwa jina la Vijana wa Yesu jana tarehe 7 Julai, 2018 lilipeleka furaha kwa kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum cha Salvatory Army kilichopo maeneo ya sabasaba Wilaya ya Temeke jijin Dar es salaam na kuwapa baadhi ya mahitaji ambayo ni muhimu hapo kituoni. Wanagroup hao walifika kituoni…

Soma Zaidi >>

Kangi Lugola alivyomzuia Kamishina wa Magereza kuingia kwenye mkutano wake

Kamishina wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa amezuiwa kuingia kwenye mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya kuchelewa kwa dakika mbili kuingia kwenye ukumbi ambako mkutano huo ulifanyika. Waziri huyo ambaye aliingia kwenye ukumbi majira ya saa 4:51 asubuhi ambapo mara baada ya kuingia aliagiza kwamba ikifika saa 5:00 mtu ambaye atakuwa hajaingia ukumbuni hataruhusiwa kuhudhulia kikao chake isipokuwa waandishi wa habari. Ilipofika saa 5:00 aliagiza mlango ufungwe na usifunguliwe kwa mtumishi yoyote wa wizara wala Kamanda yoyote kuingia labda awe mwanahabari. Ambapo…

Soma Zaidi >>

JUMA NATURE AWATAKA KINA DIAMOND KUKAA PEMBENI

JUMA NATURE AWATAKA KINA DIAMOND KUKAA PEMBENI Msanii mkongwe na miongoni mwa waasisi wa muziki wa BongoFleva, Juma Nature amefunguka na kuwaonya wasanii wa sasa kuacha tabia ya kuigana na kubweteka katika kufanya kazi zao kwa kuwa kitendo hicho kinapelekea kuua muziki. Juma Nature ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha EATV baada ya kuwepo minong’ono mingi kwa mashabiki na wadau wa muziki nchini kulalamikia vitendo vya baadhi ya wasanii kutokuwa wabunifu katika ufanyaji kazi zao “Hii ni kazi lakini wengine wanachukulia ubishoo. wasanii wanabweteka sana na hilo…

Soma Zaidi >>

TANZIA: DIWANI WA CHADEMA AFARIKI DUNIA, CHADEMA KILIMANJARO WAMLILIA.

Diwani wa CHADEMA katika Manispaa ya Moshi kata ya Mawenzi, Mhe. Hawa Mushi, amefariki dunia jioni ya jana Juni 7, 2018 akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC baada ya hali yake kuwa mbaya akitokea Hospital ya St. Joseph iliyopo mjini Moshi. Taarifa ya kifo cha diwani Hawa Mushi imetolewa na mweneyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Joseph Selasini (Mbunge) ambaye amesema amesikitishwa sana na kifo hicho, na kwamba kwa niaba ya Chadema mkoa wa Kilimanjaro anatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huo. Kwa mujibu wa…

Soma Zaidi >>

MABINGWA WA NGUMI ZA RIDHAA WAMTEMBELEA MEYA WA UBUNGO

  Mabingwa ngumi za ridhaa ambao wameshinda mataji mbalimbali ya ubingwa pamoja na medali kwa Mabondia katika Shindano la Mchezo wa Ngumi kwa mkoani Dar es Salaam, leo wamemtembelea Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Bwana Boniface Jacob na kupelekea meya huyo kujitolea kuwa mlezi wa kambi yao ya Shirikisho la Ngumi kwa Wilaya ya Ubungo. Mapema Leo tarehe 30 Mei 2018, Mabondia hao ambao walishinda mataji mbalimbali na Medali Sita(06), ambazo ni Dhahabu Moja (01), Shaba Mbili (02) na Fedha Tatu(03), walimtembelea Meya huo kama heshima kubwa sana kwa niaba…

Soma Zaidi >>