KAMPUNI YA VISA WASHIRIKIANA NA HALOTEL KULETA MALIPO YA QR KWA WATUMIAJI WA HALOPESA

  Wateja milioni 1 na wakala 40,000 kupata huduma ya malipo ya Visa kupitia Halopesa. Kampuni ya Teknolojia ya malipo ya kimataifa ya VISA imetangaza ushirikiano wa mkakati na Halotel ili kuwezesha malipo ya Visa kwenye simu kwa kutuma codi ya QR kwa wateja wa Halotel nchini Tanzania. Huduma hiyo itakayotolewa mwanzoni mwa mwaka 2019 na hivyo kuwezesha wateja zaidi ya milioni moja wa HaloPesa kutumia Visa kwenye simu ili waweze kufanya malipo ya biashara kwa salama na kuweka na kutoa fedha kwa mawakala wa Visa.Mteja yoyote wa HaloPesa, ikiwa…

Soma Zaidi >>

UBER YAZINDUA ZANA YA USALAMA KWA ABIRIA NA MADEREVA

JOHANNESBURG, Kampuni ya UBER yaongezea usalama na yatoa Zana ya Usalama kwa abiria na madereva katika nchi 8, pamoja na Tanzania; Vipengele vitajumuisha Kituo cha Usalama, Waasiliani Wanaoaminika, kitufe cha usaidizi wa dharura na taarifa kuhusu viwango vya mwendo ambavyo unaweza kuvigeuza kukufaa.  Hivi Uber imetangaza Zana mpya ya Usalama ambayo, kwa wiki chache zifuatazo, itaanza kutumiwa na mamilioni ya abiria, madereva na watoa huduma ya uwasilishaji wanaotumia programu hii katika bara Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika. Zana hii itaanzisha vipengele vipya bunifu ambavyo vinalenga kuimarisha kigezo cha usalama,…

Soma Zaidi >>

TAHADHARI: TAREHE 27 JULAI KUSHUHUDIWA TUKIO LA KUPATWA KWA MWEZI KWA MUDA MREFU ZAIDI

Taarifa kutoka kwa Shirika la Usimamizi wa Anga za Juu (NASA) zinasema kuwa siku ya kesho kutwa Julai 27, 2018, dunia itashuhudiwa tukio la kupatwa kwa mwezi, ambalo si la kawaida. Kwa mujibu wa habari iliyoripotiwa na BBC mapema siku ya leo inasema kuwa, shirika hilo limetoa taarifa inayosema tukio la kupatwa kwa mwezi mnamo siku hiyo ya Julai 27 litakuwa la muda mrefu zaidi kuwahi kutokea katika karne ya 21. Taarifa hiyo inaeleza kuwa tukio hilo litashuhudiwa kwa ukaribu zaidi katika maeneo ya Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, katikati mwa…

Soma Zaidi >>

Dubai yazindua jengo refu zaidi duniani lenye ghorofa 75

Jana Jumapili Februari 11, 2018 Dubai iliendeleza desturi yake ya kuwa na majengo marefu zaidi duniani, kwa kuzindua jengo lingine la Gevora Hotel Towers. Jengo hilo linakuwa la kwanza duniani kwa urefu kutokana na kuwa na ghorofa 75 na urefu wa mita 356 kwenda juu. Hata hivyo, rekodi ya jengo refu la hoteli duniani ilikuwa inashikiliwa na Dubai yenyewe ambapo jengo la hoteli la JW Mariott Marquis ambalo limezidiwa mita moja tu na jengo jipya la Genova Hotel ndio lilikuwa linashikilia rekodi hiyo.

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUIMARISHA TTCL ILI KUFIKIA USHINDANI KIBIASHARA

Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimarisha Kampuni ya Simu nchini (TTCL) iIi iweze kuingia kwenye ushindani wa kibiashara dhidi ya makampuni mengine ya simu. Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa shirika hilo, Waziri Kindamba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es Salaam. Kindamba alisema hayo kufuatia Novemba 14, mwaka huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadili na kupitisha miswada ya mapendekezo ya mabadiliko ya sheria yanayofuta sheria iliyounda Kampuni ya Simu ya TTCL (Tanzania Telecomunication Company, Incoporation Act 2002) na kutunga sheria…

Soma Zaidi >>

SIKIO KUTUMIKA KUFUNGUA NA KUFUNGA SIMU KAMA ILIVYO KWA KIDOLE. (EAR PRINT)

Tafiti iliyofanyika kwenye chuo cha Michigan, nchini Marekani imesema baada ya mazoea ya watu wengi kuweza kufunga simu zao kwa kutumia finger print, sasa watu wataweza funga na kufungua simu zao kwa kutumia masikio yao , yaani Ear print. Tafiti hiyo inasema kuwa mtu tapaswa kudownload application iitwayo ERGO kwenye simu yake ili aweze kupata uwezo huo kwenye simu yake, kwa kufunga na kufungua simu kutumia simu yake. Yote hayo bado yapo kwenye matengenezo ya mwisho, na kwa sasa vyote vipo kwenye mfumo wa demo.

Soma Zaidi >>

WHATSAPP WAMEKUJA NA MAAJABU MENGINE YAKUSHANGAZA.

​ Ivi Ilishawahi kukutokea kutuma ujumbe, picha au video au documenti yeyote kwa mtu usiyemkusudia kwa bahati mbaya kupitia programu ya WhatsApp? kama jibu ni ndiyo, basi sahau kabisa kukutana na maswahibu hayo tena, kwani tayari programu hiyo imeshaongeza sehemu ya kufuta jumbe hizo. WhatsApp tayari imezindua huduma hiyo ambayo imeongezwa kwenye programu kwa jina ‘Delete For Everyone’ ambapo mtumaji wa ujumbe, picha au video atachagua kufuta kwake au kwa mtu aliyemtumia kimakosa. Kwa sasa huduma hiyo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS na Android kama bado basi cha kufanya…

Soma Zaidi >>

WHATSAPP KUJA NA ‘LIVE LOCATION’ KWA WATEJA WAKE

​ Mtandao wa kijamii wa WhatsApp upo mbioni kuongeza sehemu mpya kwa watumiaji wake itakayomuwezesha mtumiaji kuonesha eneo alipo kwa muda huo (Live Location) kwa watu atakaowasiliana nao kupitia WhatsApp. Haya ni maboresho ambayo mtandao huo umedhamilia kuyafanya kwa mwaka huu ili kuendana sawa na programu nyingine kama Snapchat, Facebook, iMessanger n.k .​ Sehemu hiyo ya Live Location itakusaidia kuwaonesha marafiki, ndugu na jamaa zako sehemu uliyopo kwa dakika 15, hadi masaa 8 kutokana na wewe mwenyewe unavyotaka, lakini pia unaweza kuibadilisha kwa aidha uiweke Automatic au Manually kama ilivyo…

Soma Zaidi >>

WHATSAPP KUACHIA TOLEO JIPYA LA WHATSAPP BUSINESSES.

​ Mtandao wa WhatsApp umeachiatoleojipya la WhatsApp Business ambalo limekuja na App yake maalumu kama unavyo iona kwenye picha hapa ​ App hiyo itakuwa na uwezo wa kuwaunganisha wafanya biashara na wateja wao kwa karibu kwa njia ya biashara zaidi. Toleo hili litahitaji kwanza uweze kujisajili kwakujaza fomu ya WhatsApp, jina la kampuni, namba ya simu pamoja na nchi ambako kampuni inapatikana. Baada ya hapo WhatsApp watakutumia link itakayokufanya uweze kupakua (download) App hiyo kirahisi zaidi. ​ Bila yakufanya hivyo hutoweza kuipata App hiyo kwakuiona PlayStore wala kuifungua. Endelea kufwatilia…

Soma Zaidi >>