NIMEMPA KICHAPO NDIO …………

Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandra au maarufu kama Mama Diamond amethibitisha kumpa kipigo cha mbwa mwizi mkwe wake Hamisa Mobetto. Mwanzoni mwa wiki hii kuna stori ilisambaa kuwa Mama Diamond kampa kipigo kizito Hamisa baada ya kuwepo nyumbani kwa Diamond Madale, hadi kuacha wigi lake. Mama Diamond amethibitisha habari hizo kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers ambapo ameweka wazi kuwa hampendi na hataki hata kumuona nyumbani kwake: “Ni kweli nilimpiga na wigi nikamvua na hayo mambo ya kumfuata mzazi mwenzie ni huko, pale Madale…

Soma Zaidi >>

FAIZA HANA MALENGO NA BEBE WAKE

Faiza Ally ni miongoni mwa wanawake wenye mvuto mkubwa sana hapa Bongo. Mwanamama huyo ambaye aliwahi shiriki shindano la Big Brother Afrika, pia ameingia kwenye kiwanda cha muziki ambako pia anafanya vizuri. Kikubwa sasa ni kwamba amekuwa kimya sana katika sekta ya mapenzi tofauti na wasanii wengine wa kike. Akifunguka sababu hasa ya kutomuweka wazi partner wake huyo ni kama hivi. Mwanadada Faiza Ally amefunguka ya moyoni na kuelezea kiundani sababu gani iliyomfanya ashindwe kumuweka wazi mpenzi wake ambae ni baba wa mtoto wake wa pili, Faiza ambae amekuwa akiweka…

Soma Zaidi >>

MBASHA NA KIBA KAMA RONALDO….

Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Filauni, Yes kupitia darmpya.com we had informed you kumuhusu mkali wa ‘Mvumo wa Radi’ Ally Salehe Kiba ‘Alikiba’ kuburuzwa mahakamani kwa kushindwa kutoa matunzo ya mtoto (hayo ya Muda), Sikia ya filauni, mwimbaji wa nyimbo za injili  na mume mtalaka wa mwanamama Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha naye amekutwa na skendo kama hiyo baada ya kudaiwa kumtelekeza mwanaye mwenye umri wa miaka mitatu. kwa mujibu wa chanzo cha ndani kabisa imeelezwa hivi karibuni Mbasha aliburuzwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar na mama mtoto…

Soma Zaidi >>

FULL STORI ALIKIBA KUKATAA MTOTO

Mambo ni moto! Baada ya hivi karibuni mzazi mwenzake na staa wa Bongo Fleva, Ally Salehe Kiba ‘King Kiba’, Hadija Hassan kuuambia umma kwamba amemwaga ugali kwa kwenda mahakamani kudai malezi ya mtoto, utata mkubwa umeibuka katika kesi hiyo. Kinachotatiza ni pale King Kiba naye alipoibuka ‘juzikati’ mbele ya ‘maiki’ ya redio maarufu jijini Dar na kumwaga mboga kuwa hajui chochote kuhusu kesi inayoelezwa na Hadija kwenye vyombo vya habari kuhusu yeye kumtelekeza mwanaye. “Yule mtoto kweli ni wa kwangu, ugomvi wetu unakuja pale familia yetu tunapotaka kumchukua na kukaa…

Soma Zaidi >>

NYUMA YA PAZIA SABABU ZA LULU KUTOKA GEREZANI

Kukidhi vigezo vya kisheria pamoja na kuonesha tabia njema ni miongoni mwa sababu za msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’ kubadilishiwa kifungo cha kukaa gerezani ambapo kwa sasa anatumikia adhabu hiyo akiwa nje (kifungo cha nje), zilizotajwa na Idara ya Magereza nchini. Idara ya Magereza kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo, imesema Lulu amebadilishiwa adhabu hiyo kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Dar es Salaam. Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela mwezi Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia katika kesi iliyokuwa inamkabili ya…

Soma Zaidi >>

NANDY AAPA KUTOONGEA NA VYOMBO VYA HABARI

Msanii wa muziki wa bongo fleva anayejulikana kwa jina la Nandy (the African Princess) ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram kuwa kwa sasa hatoongea tena na vyombo vya habari kuhusiana na kuvuja kwa video  inayomuonyesha akiwa faragha na msanii mwenzake bill Nas. Nandy ameandika kuwa kwa sasa yupo katika wakati mgumu sana  “maswali ni mengi matusi ni mengi simu na sms ni nyingi mnoo… naumiaa naumiaa kupita kiasi. Kanisaa langu, wazazi wangu, ndugu zangu, marafiki zangu wa karibu wameliaa sana sanaa mnoo!!! sikatai nimerecord video na nilikuwa kwenye mahusiano na nilifanya…

Soma Zaidi >>

KIGOGO WA CCM ADAIWA KUTAKA KUMUUA MTOTO WA NJE YA NDOA ILI KUFICHA SIRI

Katibu wa CCM Kata ya Kitangili iliyopo Manispaa ya Shinyanga, Edson Timotheo Damian anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kutaka kujaribu kumuua mtoto wake wa miezi miwili aliyezaa na mwanamke wa nje ya ndoa. Tukio hilo limethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Simon Haule, na kusema kuwa upelelezi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili. Akielezea kuhusu tukio hilo, Mama wa Mtoto huyo, Maria Shija amedai kuwa tukio hilo lilitokea Machi 24, 2018 ambapo mtuhumiwa alikwenda nyumbani kwake kwa ajili…

Soma Zaidi >>

MTEGO WA ZARI WANASA KWA MOBETTO

Mwanamitindo Hamisa Mobeto anadaiwa kunasa mtegoni baada ya ‘kuuvaa mkenge’ ulioratibiwa na hasimu wake wa siku za hivi karibuni,Zarinah Hassan ‘Zari’. Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Zari, inadaiwa kuwa mjasiriamali huyo alimtumia mtu aitwaye William Bugeme ambaye pia ana ukaribu naye wa damu, ili aweze kumchukua mwanamitindo huyo, ambaye amezaa na baba wa watoto wake wawili. Inadaiwa lengo la Zari ni kuona wawili hao wakiwa karibu, basi ni dhahiri kuwa ukaribu kati ya Hamisa na baba watoto wake utaisha, kwani uhusiano wa kimapenzi na William hauwezi kukubalika. “Mnajua…

Soma Zaidi >>

KAMIKAZE APINGA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MPENZI WAKE FEZA KESSY

Star wa Bongo Fleva Cyril Kamikaze amefunguka kuhusu tuhuma zinazomkabili za kumdhalilisha mpenzi wake Feza Kessy kwa kuanika picha inayoonyesha matiti yake katika mtandao wake wa instagram. Kamikaze amesema haoni tatizo lolote la ile picha kwani ni picha ya kawaida sana na haijaonyesha kiungo chochote cha Feza anachojua ni kwamba picha ile inaonyesha sehemu kidogo ya matiti ya Feza ambapo ni sawa tu na wanawake wanaovaa brazia kuyabusti maziwa yao ili yaonekane. Hata hivyo Kamikaze amesema hawezi kumdhalilisha Feza kwani anamuheshimu sana na Feza ndo alipiga ile picha na kumtumia…

Soma Zaidi >>

KAMIKAZE APINGA TUHUMA ZA KUMDHALILISHA MPENZI WAKE FEZA KESSY

Star wa Bongo Fleva Cyril Kamikaze amefunguka kuhusu tuhuma zinazomkabili za kumdhalilisha mpenzi wake Feza Kessy kwa kuanika picha inayoonyesha matiti yake katika mtandao wake wa instagram. Kamikaze amesema haoni tatizo lolote la ile picha kwani ni picha ya kawaida sana na haijaonyesha kiungo chochote cha Feza anachojua ni kwamba picha ile inaonyesha sehemu kidogo ya matiti ya Feza ambapo ni sawa tu na wanawake wanaovaa brazia kuyabusti maziwa yao ili yaonekane. Hata hivyo Kamikaze amesema hawezi kumdhalilisha Feza kwani anamuheshimu sana na Feza ndo alipiga ile picha na kumtumia…

Soma Zaidi >>