WAZIRI KIGWANGALLA NA WAKILI KARUME WAWEKA HISTORIA

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt.Hamis Kigwangalla amekutana na kufanya kikao chake cha chakula cha mchana na Wakili Fatuma Karume kujadili jinsi ya kuboresha uhusiano baina ya viongozi wanapowasiliana kutumia mitandao ya jamii na kuwa mfano bora kwa vijana wanaochipukia kwenye uongozi. Kupitia ukurasa wake wa twitter, Waziri Kigwangalla ameandika kuwa, “ Tuache utani pembeni, Siasa pembeni. Kuna la kujifunza katika hadithi hii; Shangazi ni mtu poa sana, mnyenyekevu, mvumilivu, msikivu, mwenye uelewa mpana wa mambo, na anasababu zake katika kila anachokifanya. Aidha Kigwangalla amesema, mkutano huo unatoa funzo kwa…

Soma Zaidi >>

ANATAKA UMAARUFU KUPITIA MIMI WALA SIKUMBAKA: RONALDO

Na Jyross Curtis Mchezaji bora na ghari duniani katika dimbwi la soka, Cristiano Ronaldo, amekana madai ya mwanadada Kathryn Mayorga alietoa madai ya kubakwa na Ronaldo mnamo mwaka 2009 katika moja ya hoteli jijini Las Vegas, Marekani. Staa huyo wa kandanda alionekana katika video yake ya Instagram akikataa madai ya mwanamke huyo kwa kusema “Wanataka umaaruufu kupitia jina langu, ni kawaida yao”. Hata hivyo mawakili wa Ronaldo nao hawakupendezwa na taarifa hiyo iliyotolewa kupitia jarida la ujerumani la Der Spiegel na hivyo basi wameamua kulishitaki kwa kuripoti madai hayo ysiyo…

Soma Zaidi >>

MCHUNGAJI TITO MWINGINE WA ZIMBABWE AKAMATWA NA POLISI KWA KUUZA TIKETI ZA KWENDA MBINGUNI

HARARE. Hakika Dunia ina mambo tena sana na binadamu katika enzi hizi hutumia kila mbinu kuhakikisha anavuna kutoka kwa mwenzake, huko nchini Zimbabwe Mchungaji mmoja amekamatwa na jeshi la polisi alipokuwa akiwauzia tiketi waumini wake akisema zitawawezesha kuingia mbinguni. Pasta huyo aliyejulikana kwa jina la Tito Wats, pamoja na mke wake wamekuwa wakiwauzia kondoo wake tiketi za kwenda mbinguni kwa Dola 99.4 sawa na zaidi ya Tshs Laki Mbili na Elfu Ishirini. Kulingana na mchungaji huyo, Yesu alimjia binafsi na kumshauri aanze kuuza tiketi hizo. Mbinu iliyotumiwa na mchungaji mmoja wa Zimbabwe…

Soma Zaidi >>

MAITI AZUNGUMZA KABLA YA KUZIKWA, AMTAJA ALIYEMTOA KAFARA

MACHAKOS. Watu wengi waliohudhuria mazishi walisalia vinywa wazi kusikia sauti kutoka kaburini, baada ya mwili wa msichana mmoja aliyekuwa kafariki katika ajali ya barabarani kumtaja mjomba wake kuwa ndiye aliyetumia kafara kumuua ili atajirike Maeneo ya Masii, Machakos nchini Kenya, kilizuka kioja katika mazishi ya mwanadada huyo aliyefariki katika ajali ya barabarani. Inadaiwa kuwa mwanadada huyo mwenye umri wa miaka 27 alikuwa akiishi na mjomba wake mjini Voi kabla ya kifo chake. Kulingana na kisa hicho kilichochapishwa katika gazeti la “Taifa Leo” la nchini humo, mwanadada huyo alifariki katika ajali…

Soma Zaidi >>

RAIS WA UFARANSA AZUA MIJADALA BAADA YA KUMBUSU HADHARANI RAIS WA CROATIA

Rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarovic amezua mijadala mtandaoni baada ya kuonekana kwenye kamera akipigwa busu na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, hii ilikuwa wakati Ufaransa ilishinda Kombe la Dunia la 2018 juzi Jumapili Julai 15. Bi. Kitarovic amezungumziwa sana ulimwengu mzima kwani amekuwa shabiki sugu wa michuano yote ya Kombe la Dunia ya mwaka huu, kwa sababu alionekana kila mara akiwatia moyo wachezaji wake, jambo lililowafurahisha wengi Kolinda alisisimua mitandao ya kijamii hapo Jumapili siku ya fainali baada ya kuonekana kwenye kamera akipigwa busu na Rais mwenzake wa Ufaransa, Emmanuel…

Soma Zaidi >>

AMUUWA MUMEWE KWA KISU KISA CHAKULA

Sophia Salehe, mkazi wa Kata ya Namiongo, Newala mkoani Mtwara, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa tuhuma za kumuua mume wake kwa kumchoma kwa kisu. Mauaji hayo yalitokana na ugomvi baina ya mtuhumiwa ambaye inadaiwa kuwa alikataa wito wa mumewe kupika chakula baada ya kutokushiba. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Lucas Mkondya, amesema tukio hilo lilitokea juzi mkoani humo. Kwa mujibu wa Mkondya, mwanamume huyo alikufa papo hapo baada ya kuchomwa kisu na mke wake. Alisema siku ya tukio majira ya saa 1:30 usiku, mwanamke huyo alimwandalia…

Soma Zaidi >>

MBARONI KWA TUHUMA ZA KULAWITI WATOTO WATATU

Mwanaume mmoja anayejulikana kwa jina la Mohamedi Kaisi Hamisi mwenye miaka 47 mkazi wa kijiji cha Kawawa mkoani Mtwara, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma za ulawiti. Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara Lucas Mkondya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba mwanaume huyo anatuhumiwa kulawiti watoto watatu wenye miaka 13, 14 na 15, wa shule ya msingi Kawawa, walipokuwa wanatafuta Nazi kwenye minazi iliyopo vichakani baada ya kutoka Kamanda Mkondya amesema kwamba baada ya kuwakuta watoto hao mtuhumiwa aliwatishia maisha kabla ya kufanya kitendo hicho cha…

Soma Zaidi >>

MIL. 250 ZA SHEIKH ZILIVYOMFIKISA MAHABUSU MENEJA WA DIAMOND ‘BABU TALE’

Meneja wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, Hamis Taletale maarufu kama Babu Tale amefikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam akiwa chini ya ulinzi kwa ajili ya kusikiliza kesi ya madai iliyofunguliwa mahakamani hapo na Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hamis Mbonde. Babu Tale katika kesi hiyo yuko pamoja na ndugu yake Iddi Taletale  ambapo Mahakama hiyo iliwamuru kumlipa Sheikh Mbonde kiasi cha Sh. Milioni 250 baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo ya sheikh huyo kibiashara bila ridhaa yake…

Soma Zaidi >>

WCB KWACHAFUKWA

Unakumbuka ile big ishu ambayo ilitrend kwa kitambo fulani kufikia hatua kumpeleka Nandi mahakani?. Naongelea Ishu ambayo ilihusisha kuvuja kwa video ambayo ilitafsiriwa kuvunja maadili ya kitanzania kwa kusambaza mambo ya faragha hadharani. Video hiyo ilikuwa ikimuonyesha Nandi na msanii mwenzake Bilnas katika mazingira tatanishi ya kimahaba chumbani. Moja kati ya mambo mengi na fikra nyingi kutoka kwa fans wa industry ya entertainment ni kwamba waliamini Nandi alifanya hivo kwa ajili ya kiki japo alikanusha ya kwamba hakuwa akifahamu chochote juu ya chanzo cha kuvujisha video hiyo. Time zimekwenda na…

Soma Zaidi >>

WASTARA ANAONEWA JAMANI

Msanii wa kike wa filamu Bongo Wastara Juma amefunguka juu ya picha aliyopost instagram na kuzua mjadala kwa baadhi ya watu, huku wakimtuhumu kupanga njama za kutapeli kwa kutumia ugonjwa wake, ambao ulikuwa unamsumbua muda mrefu na kusababisha kupelekwa India kwa matibabu. Akizungumza na www.eatv.tv Wastara amesema kwamba kitendo cha watu kumfikiria vibaya  kinamtia uchungu na kinamvunja moyo, kwani ukizingatia hakuomba kupata matatizo aliyopata, na kwamba picha aliyopost ni ya muda mrefu akiwa nchini India. “Kwa kweli inasikitisha na inavunja moyo sana kama Mtanzania, na kama mtu ambaye nina haki…

Soma Zaidi >>